In Summary

• Musila aliahidi kuendelea kumpenda mumewe licha ya kuwepo kwa pingamizi nyingi kutoka kwa mashabiki wao kutokana na utofauti mkubwa uliopo baina ya miaka yao.

Esther Musila, Guardian Angel wabemendana kwa mahaba
Image: INSTAGRAM

Guardian Angel na mkewe Esther Musila wanazidi kupapatiana na kubembendana mitandaoni kwa mapenzi yasiyojua kufa.

Angel alipakia pichayake mpya kwenye Instagram yake akiwahimiza mashabiki wake kuwa kila siku iendayo kwa Mungu wanafaa kujitahidi kutokea tofauti, katika kile alisema kuwa mtu tofauti siku zote huonekana na wengi.

Mkewe, Musila alichukua picha hiyo na kuipakia kwenye ukurasa wake akimsifia na kumetipeti Angel akimshukuru kwa kuleta mwanga wa nuru katika maisha yake.

Musila aliahidi kuendelea kumpenda mumewe licha ya kuwepo kwa pingamizi nyingi kutoka kwa mashabiki wao kutokana na utofauti mkubwa uliopo baina ya miaka yao.

“Asante kwa kuleta furaha kwa moyo wangu, uzuri kwa ulimwengu wangu, na upendo kwa maisha yangu. I loooove you Bw Omwaka,” Musila aliandika.

Kama hilo halitoshi, Angel alifika kwenye chapisho hilo la picha yake na kuongezea uzito kwenye maneno ya huba ya mkewe akimwambia kwamba hapatatokea mtu yeyote kuwa kivuruge katika penzi lao.

“Unajua wewe ni Kila kitu kwangu. nakupenda Zaidi,” Guardian Angel alisema.

Wawili hao walioana mwanzoni mwa mwaka 2022 katika hafla ya harusi ya faraghani na licha ya kuwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya mashabiki wao mitandaoni, wamezidi kuwapakulia wabaya wao mchuzi moto kwenye kikombe cha mabati.

View Comments