In Summary

• Alisema kuwa tukio hilo lilikuwa kati ya maudhui yake ambayo alikuwa amepanga kufanya siku hiyo.

• "Mimi nilikuwa nimeambia umati hivyo kwamba nimekuja na chupi na sidiria zangu, nataka kuwapatia mnitupie,”

UGANDA Erick Omondi akiri kuwataka watu wamtupie chupi
Image: INSTAGRAM

Mchekeshaji Erick Omondi kwa mara ya kwanza amezungumzia tukio la aibu ambalo lilimtokea akiwa anatumbuiza nchini Uganda katika tamasha la Comedy Store lililohudhuriwa na watu wengi akiwemo msanii Diamond Platnumz.

Katika mahojiano kwa njia ya Simu na mwandishi Moses Sagwe kutoka tovuti ya Radio Jambo, Omondi alikiri madai ya baadhi ya watu mitandaoni kwamba ni tukio ambalo alikuwa ameliratibu mwenyewe.

Mchekeshaji huyo ambaye amegeuka kuwa mwanaharakati alisema kwamba japo aliwapanga vipusa hao katika sehemu Fulani za ukumbi huo ili kumtupia chupi, hakuwalipa ili kufanya hivyo.

Alisema kuwa tukio hilo lilikuwa kati ya maudhui yake ambayo alikuwa amepanga kufanya siku hiyo na anashukuru Mungu lilizaa matunda jinsi ambavyo alikuwa ameratibu.

“Ni kweli si hiyo ndio kazi yangu. Sikuwalipa si hiyo klipu iko. Si unajua Erick Omondi ni mchekeshaji. Hiyo ndio joke. Watu hawakuelewa hiyo joke. Ilikuwa ndio ukitaka kujua kama msanii anapendwa, lazima atupiwe chupi na sidiria. Mimi nilikuwa nimeambia umati hivyo kwamba nimekuja na chupi na sidiria zangu, nataka kuwapatia mnitupie,” Omondi alisema.

Mchekeshaji huyo alisema kuwa shoo hiyo ilifanikiwa pakubwa na kufichua kwamab ilikuwa na umati wa watu elfu 15 waliohudhuria.

Awali katika msururu wa mahojiano hayo, Omondi alifichua kwamba ana mpango wa kuingia katika siasa ili kupata nafasi kubwa ya kuendeleza harakati zake za kuwapigania watu wenye maisha ya nchini.

Pia alisema kwamba nchini Uganda hakuweza kufanya mchango wake wa omba omba aliouita ‘woiyee tour’ katika kile alisema kwamba alifika kuchelewa nusra kuachwa na ndege.

View Comments