In Summary

• Mtangazaji huyo alisema kwamba ni yeye alikuwa wa kwanza kumwambia Bonez kwamba wangekuwa wapenzi.

MAPENZI Kamene afunguka mara ya kwanza kuutana na Bonez.
Image: screengrab

Mtangazaji Kamene Goro amefunguka jinsi walikutana na mpenzi wake Dj Bonez kwa mara ya kwanza.

Katika podkasti yake na mchekeshaji Oga Obinna, Kamene alieleza kwamba kipindi wanakutana na Bonez, alikuwa mdogo kama miaka 25 hivi na mcheza santuri huyo alikuwa anamchukia sana kwa kumuona kama mzinzi – ratchet kwa kimbombo.

“Tulikutana Mombasa, na mimi na yeye hatukupendana kwa mara ya kwanza. Nilikuwa na kama miaka 25. Tulikuwa kwenye klabu na mtangazaji mwenza na Bonez alikuwa ananichukia. Kwanza alikuwa anadhania mimi ni mzinzi kama huyo mwenzangu,” Kamene alisema.

“Lakini ulikuwa…..” DJ Bonez alimkatisha kwa haraka.

Kamene alijitetea akisema kwamba hakuwa mzinzi bali ni vile alikuwa mdogo la ni vile alikuwa anakaa na huyo mtangazaji mwenza mwenye tabia ambayo ilikuwa inamuonesha kama mzinzi.

“Kipindi hicho alikuwa ananichukia mbaya licha ya kwamba nilikuwa hotcake, nilikuwa na short blonde hair halafu nilikuwa mwembamba,” Kamene aliongeza.

“Kwa muda mrefu tulikuwa katika kundi moja lakini hatukuwahi ongea kwa sababu yeye alichukulia kwamba niko kama huyo mwenzangu hadi Desemba 2020.”

Mtangazaji huyo alisema kwamba ni yeye alikuwa wa kwanza kumwambia Bonez kwamba wangekuwa wapenzi.

“Ni mimi nilimkatia. Unaona tulikuwa tunaenda kwa hoteli kila siku tunajivinjari na nilipata gigs nyingi Januari Mombasa na kila wikendi ilikuwa inanibidi lazime niwe Mombasa. Hapo tukaanza kuongea kwa DM sana nikamwambia sasa toka DM twende WhatsApp,” alisema.

View Comments