In Summary

• "Kuna muda nilipiga zoezi nikapunguza kilo 13 za uzani na nikaenda Marekani kwa wiki mbili tu nilirudi kama nimeongeza kilo 6,” Raburu alikumbuka.

Raburu kuhusu kuongeza uzani.
Image: Facebook

Aliyekuwa mtangazaji wa runinga ya Citizen, Willis Raburu amezungumzia tabia yake ya kuwa na furaha na mihemko mingi haswa anapokuwa katika hali ya hadhara.

Raburu ambaye alikuwa anazungumza na Director Phil kwenye podkasti yake alisema kuwa yeye ni mtu ambaye kukasirika kwake ni kugumu sana hata katika familia, kazini na mahali pengine popote.

Alisema kwamab alijifunza kukumbatia tabia hiyo ya kuficha matatizo yake ndani ya blanketi la furaha baada ya kupitia mambo mengi mitandaoni kutoka kwa watu ambao walikuwa wanamwambia maneno yasiyofurahisha kuhusu kuongeza uzani wa mwili.

Raburu alisema tangu akumbatie hulka hiyo, si rahisi kumpata akiwa amekasirika.

“Mimi kijumla nilikuwa napenda kuwa mtu mkimya. Mim ni msee nilikuwa nachukua mateso.. unajua ule wimbo ‘mateso ni ya roho’… mimi sikuwa naongea, haikuwa inakuja kwa mdomo. Mimi nilikuwa nameza hasira hata kama ni kazini, kwa familia, popote. Nitachukua chochote. Yaani kwangu mimi kunipata nimekasirika ni vigumu sana, lakini pengine kama niko njaa. Lakini kukasirika nako kunanichukua muda mrefu sana,” Raburu alisema.

Raburu katika kusimulia maisha yake ya kuongeza na kupoteza uzani wa mwili kupitia upasuaji, alisema kuwa kwa muda mrefu watu walimshambulia mitandaoni mpaka akafika hatua ya kutaka kukata tamaa na mwili wake mwenyewe.

“Ilikuwa inanipa msongo wa mawazo, inaniumiza na iliniingia mara nyingi sana, wakati mwingine nilikuwa napakia picha tu kujifurahisha lakini komenti za watu zilikuwa zinanikata kabisa. Kwangu mimi nafikiri ninaongeza uzani tu kutokana na kula sana kupunguza stress. Kuna muda nilipiga zoezi nikapunguza kilo 13 za uzani na nikaenda Marekani kwa wiki mbili tu nilirudi kama nimeongeza kilo 6,” Raburu alikumbuka.

“Niliongeza uzani mwingi 2020 kutokana na kula sana kuondoa stress. Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu kutoka kupoteza mtoto, kutalikiana, niliongeza uzani mwingi sana. Nilikuwa nahisi kuongeza uzani wangu kwa sababu kwa kiti nilipokuwa naketi kula na najihisi kabisa naongeza uzani,” alieleza.

“Ikifika muda mtu ameongeza uzani kupita kiasi anajua, na wengi huwa hawana furaha nayo, wanajaribu kuwa chanya kama wawezavyo lakini katika akili zao wanajua wanahitaji kufanya jambo.”

 

View Comments