In Summary

• Shabiki huyo alionekana kuashiria kuwa msingi wa mahusiano baina ya mwanamuziki huyo na Nyamu ulikuwa ni hela na si mapenzi.

• Samidoh alieleza hiyo ilikuwa baadhi ya misemo wanazozitumia watu wenye gere kuelekea kwa watu walio katika mahusiano ama wanaofanikiwa kimaisha.

Samidoh
Image: Facebook//Samidoh

Mwanamuziki wa nyimbo za Mugithi, Samuel Muchoki almaarufu Samidoh amemjibu shabiki aliyekuwa akidai kuwa alikuwa kwenye mahusiano na Seneta maalum, Karen Nyamu sababu ya hela.

Shabiki huyo alionekana kuashiria kuwa msingi wa uhusiano baina ya mwanamuziki huyo na Nyamu ulikuwa ni hela na si mapenzi.

"Samidoh hapendi Nyamu anapenda pesa zake," shabiki huyo alifunguka.

Jibu la neno moja kutoka kwa Samidoh uliwaacha mashabiki mdomo wazi wengi wakiichukulia kama njia yake ya kulenga mabishano mitandaoni.

"Joh" lilisoma jibu hilo la Samidoh liliyoambatanishwa na emoji za kucheka.

Samidoh alieleza hiyo ilikuwa baadhi ya misemo wanazozitumia watu wenye gere kuelekea kwa watu walio katika mahusiano ama wanaofanikiwa kimaisha.

Wanamitandao wengi wamekuwa wakiibua gumzo mitandaoni kuhusiana na mahusiano baina ya mwanamuziki huyo kutoka kaunti ya Nyandarua na wakili Nyamu kwani Samidoh ni mume wa Edday Nderitu.

Mapema mwezi huu, seneta Nyamu alibainisha kuwa ni maombi yake kwamba mpenzi wake Samidoh atakuja kuungana tena na familia yake na Edday Nderitu ambayo imekuwa ikifurahia muda nchini Marekani.

Wakili huyo alithibitisha kuwa ni maombi yake kuwa siku moja Edday atarudi nyumbani ili wawe familia moja kubwa.

Nyamu alikuwa amechapisha nukuu kuhusu kuwasaidia wengine wakati mke huyo wa mzazi mwenzake alipofanywa kuwa mada.

View Comments