In Summary

• Willis Raburu ameelezea jinsi mpishi mmoja katika hoteli moja nchini alimkejeli kwa sababu ya kuwa mnene.

• Willis alifichua kuwa baada ya kuacha kazi yake katika Runinga ya Ctizen sasa alikuwa amepata kazi katika ofisi ya gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja.

Willis Raburu katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Mtangazaji wa zamani wa runinga ya Citizen TV Willis Raburu ameelezea jinsi mpishi mmoja katika hoteli moja nchini alimkejeli kwa sababu ya kuwa mnene.

Raburu akizungumza na muunda filamu maarufu Phil Director siku ya Jumatatu, alieleza alipokuwa akielekea kupanda lift kuelekea katika ghorofa ya juu katika jumba la hoteli hiyo mpishi huyo alimzuia kutumia lift akisema kuwa uzani wake ungefanya lift kujaa.

"Nakumbuka wakati mmojaa nlikuwa katika hoteli moja inayotambulika mjini na tulikuwa tunaingia lift. Mpishi moja out of nowhere akashout ahh wewe usiingie unajua ukiingia hii lift itajaa."

Willis alieleza kuwa siku hizi kejeli za wanamitandao  kuhusiana na uzani wake hazimuathiri kama hapo awali na sasa hakukubali kupigwa picha na wafuasi wake mitaani.

"Watu walikuwa wanakuja kupiga picha na mimi alafu wananiabia vile imi ni mnene, lakini ilifika time nikaacha kupiwakataza. Mtu akikuja tupige picha nakataa tu kwa sababu sikuhisi vizuri na mwili wangu."

Hivi majuzi, Willis alijitokeza na kueleza alikuwa amefanyiwa upasuaji wa kupunguza uzani. Kulingana na Willis upasuaji huo ulimgharimu zaidi ya kia ya shilingi laki 800.

Katika mahojiano hayo hayo, Willis alifichua kuwa baada ya kuacha kazi yake katika Runinga ya Ctizen baada ya kuhudumu kwa muda wa miaka 13 sasa alikuwa amepata kazi katika ofisi ya gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja.

Alieleza kile ambacho atafanya sasa baada ya kuacha kazi yake kwenye runinga ni kuweza kuleta mabadiliko kwa watu kwa jumla.

"Langu kuu sasa ni kutumia nafasi yangu kwa jamii kuinua watu wengine katika jamii ili waweze kufika mahali mimi mwenyewe nilikuwa tu. Najiuliza kila siku nitatumia aje hii fursa niko nayo na vile tu nimesema ni kuwasaidia waanii na watu waote kufikia umma."

View Comments