In Summary

• Musila alisema kuwa mtu yeyote ambaye anataka kufa mapema angali kijana basi sumu rahisi ni kuchanganya umaskini na wivu lakini pia kuongezea ushindani.

Musila awajibu vikali wanaofuatilia penzi lake na Angel
Image: INSTAHRAM

Esther Musila kwa mara nyingine amewapiga kwenye nyigu wanaozidi kulivalia njuga suala lake la kifamilia, kuhusu mapenzi yake na mumewe Guardian Angel.

 Safari hii Angel ametumia meme kuwasuta wengi wanaokosoa mapenzi yake na mumewe kwa kisingizio cha utofauti mkubwa wa kiumri ulioko baina yao.

Musila alisema kuwa watu wengi wanaomtupia maneno yasiyo na maana ni wale wamechanganya umaskini na wivu, akisema kuwa mchanganyiko wa hulka hizo mbili ni hatari kwa afya ya mtu.

Musila alisema kuwa mtu yeyote ambaye anataka kufa mapema angali kijana basi sumu rahisi ni kuchanganya umaskini na wivu lakini pia kuongezea ushindani.

“Kama unataka kufa mapema, changanya umaskini na wivu halafu uongeze ushindani. Utakufa kifo cha kimya kimya hata madaktari hawatobaini kiini cha kifo chako,” Musila alisema.

Hii inakuja siku chache tu baada ya Musila kumjibu kwa shombo shabiki aliyemwambia ajiweke kwenye kiatu cha mvulana wake kuoa mwanamke aliyemzidi umri mara dufu.

"Itakuwaje kama mwanao siku moja atakuletea mke ambaye ni mkubwa kuliko yeye utafeel aje?" mtumizi mmoja wa Tiktok alimuuliza.

“Huyo atakuwa mwanangu ambaye atamleta na si wako, basi isikusumbue. Kuwa na wasiwasi kuhusu fedha zako, visigino vilivyopasuka, uhusiano, kuwa na shughuli nyingi,” Musila alijibu.

Musila na Guardian Angel wamekuwa kwenye ndoa rasmi kwa mwaka mmoja na miezi kadhaa sasa lakini wanamitandao na jamii kwa baadhi hawajawahi tulia na kukubali kuwa penzi la wawili hao liko sawa na ni la kuigwa.

Wengi wamekuwa wakiwakosoa vikali wakisema kuwa Musila na Angel hawapaswi kuwa wanandoa kwani utofauti baina ya umri wao ni miaka kama 20 hivi.

Wawili hao katika kujibu, wamekuwa wakisema kuwa wengi wanaowashambulia mitandaoni ni maskini hata siku moja hawawezi kufikia maisha yao ya kifahari ambayo wanaishi, Angel kwa wakati mmoja akijibu kwamba ndiye msanii pekee wa injili anayeishi Karen.

View Comments