In Summary

• Alikiba amekuwa akitumia kauli fiche kumshambulia Diamond kupitia mtandao wa Twitter.

• Harmonize naye hajaachwa nyuma katika kuendeleza ushindani wa kibabe, akisisitiza kwamba ndiye msanii namba moja mfalme wa Bongo Flava.

Alikiba aikubali ngoma ya Diamond kwenye chimbuko la Bongo Flava.
Image: Instagram

Muziki wa Bongo Fleva umepata msukumo mkubwa kukiwa na uchachu wa mihemko baina ya wasanii mbali mbali haswa katika mwezi huu wa Julai.

Ikumbukwe Diamond ndiye alianzisha uchachu huu kwa kutangaza kwamba Julai angerejea kwa kishindo kikuu kwa kile alichokiita mvua ya mawe, akisema kwamba angeshikilia usukani wa trends hadi Januari mwakani.

Kama haitoshi, hii ilikuwa filimbi kwa wenzake ambao walkuwa wamelala katika usingizi wa pono.

Baada ya Diamond kuja kitofauti na nyimbo kwa mfululizo, hilo limewachochea maadui wake wakubwa, Alikiba na Harmonize nao kuchemka kama mvinyo wa kiasili uliotiwa hamira.

Alikiba kwa mara ya kwanza naye amekuja na mbwembwe akijaribu kupiga promo ngoma yake ya Sumu aliyomshirikisha Marioo – hali ambayo si ya kawaida kutoka kwa msanii huyo ambaye wengi wnamuona kama mhafidhina.

Alikiba amekuwa akitumia kauli fiche kumshambulia Diamond kupitia mtandao wa Twitter, haswa akionekana kufuma pale ambapo ulegevu wa Diamond unatumbuliwa.

Harmonize naye hajaachwa nyuma katika kuendeleza ushindani wa kibabe, akisisitiza kwamba ndiye msanii namba moja mfalme wa Bongo Flava.

Siku moja tu baada ya Diamond kudai kwamba ataiheshimisha tasnia ya muziki wa Bongo Flava kwa kufunga kuachia kolabo mbili mwezi Agosti akiwashirikisha Wasanii wa Marekani, Harmonize naye amelenga kule kule na kwenda mbele Zaidi kumtaja msanii mkubwa Zaidi duniani, Nicki Minaj na kudai kuwa ana ngoma naye.

Wadau wa muziki wanadai kwamba hatua ya Harmonize kumtaja msanii mkubwa anayefanya ngoma naye ni kama kutupa dongo kwa Diamond akimtaka naye kuwataja wasanii hao wa Marekani anaodai kuwa na collabo nao na ambayo inatoka mwezi ujao.

Mzungumko huu wa uchachu mitandaoni umesalia kuwa mashambulizi ya kinyume nyume baina ya Diamond na wasanii wenzake, Harmonize na Alikiba wakiwa katika mstari wa mbele kuongoza vikosi vya wabaya wa Simba wa Tandale.

View Comments