In Summary

• Itakumbukwa miaka kama 4 iliyopita Muhando alipatwa na moja ya sakata kubwa kabisa lililomleta cnhini Kenya na kujipata katika kanisa la mchungaji James Ng’ang’a.

• Kipindi hicho, Muhando alionekana kuwa mgonjwa sana mpaka kuchomeka mkono wake na wengi waling’aka wakisema kuwa alikuwa ameingia katika dini za kishetani.

YOUTUBE: Rose Muhando awa msanii wa kwanza wa injili kukanyaga subscribers milioni moja.
Image: INSTAGRAM

Rose Muhando, malkia wa muziki wa injili katika ukanda wa Afrika mashariki kwa miongo miwili sasa amekuwa msanii wa kwanza katika ukanda huu kufikisha wafuasi milioni moja kwenye chaneli yake ya YouTube.

Cha kufurahisha na kuonesha upekee wake Zaidi ni kwamba Muhando amefikisha wafuasi kwa kimombo ‘Subscribers’ miloni moja ikiwa ni miaka minne tu baada ya kuanzisha chaneli hiyo.

Mama huyo anazidi kutamba na albamu yake ya Secret Agenda aliyoitoa miezi saba iliyopita, ngoma ya Secret Agenda ikiwa mpaka sasa imejizolea utazamaji wa milioni 13.

Rose Muhando anakuwa msanii wa injili wa kwanza kabsa kuwahi kutokea na kutamalaki katika vizazi tofauti ikiwa alianza kabla ya ujio wa mitandao ya kijiditaji ya kupakua miziki na mpaka sasa anazidi kuwapa muongozo wasanii wa kizazi cha dijitali.

Itakumbukwa miaka kama 4 iliyopita Muhando alipatwa na moja ya sakata kubwa kabisa lililomleta cnhini Kenya na kujipata katika kanisa la mchungaji James Ng’ang’a.

Kipindi hicho, Muhando alionekana kuwa mgonjwa sana mpaka kuchomeka mkono wake na wengi waling’aka wakisema kuwa alikuwa ameingia katika dini za kishetani.

Baada ya Ng’ang’a kumfanyia maombi katika kanisa lake, video hiyo ilisambaa ikielezewa na baadhi kuwa ni ya kiki lakini Muhando baadae alikuja kumshukuru mchungaji huyo mtata kwa kile alisema kuwa aliokoa maisha yake.

Kwa maneno yake, Muhando alisema kwamba video hiyo ya kuombewa na mchungaji Ng’ang’a ndio iliwafanya watu wengi kujua kwamba ana matatizo na wengi kujitokeza kusimama naye kwa namna mbali mbali.

Ilisemekana kwamba aliyekuwa rais wa Kenya kipindi hicho Uhuru Kenyatta alimuonesha ukarimu mkubwa wa kumpa msaada wa kimatibabu hadi alipopona na kurejea nchini Tanzania kuanza upya uimbaji wa injili.

Alitunga wimbo mmoja akimsifia Kenyatta na taifa la Kenya kwa jumla kwa ukarimu na mapenzi waliyomuonesha kipindi alikuwa ametengwa na kila mtu karibu naye.

Tangu hapo, Muhando alijikung’uta mavumbi, Muhando alizaliwa upya na kurejea katika ubora wake kufanya injili na miaka minne baadae, ameona matunda ya kutokubali kukata tamaa wakati dunia yote ilionekana kuporomoka kwenye mwanzi wa pua lake.

Hongera sana Malkia Rose Muhando!

View Comments