In Summary

• Esma aliandika ujumbe uliowaacha mashabiki wake katika njia panda akionekana kuashiria kwa asilimia kubwa kwamba huenda mambo si shwari katika huba lake.

Esma adokeza kuachwa.
Image: Instagram

Dadake Diamond Platnumz, Esma ni mtu anayeonekana kutokuwa na kismati katika bahari telezi ya mapenzi.

Ikiwa ni miezi miwili tu baada ya  Esma kuonesha furaha yake kwa mpenzi mpya kuchora tattoo ya jina lake, mrembo huyo mama wa watoto watatu tayari ameonekana kujawa na kitunguu machoni.

Kama kile alichokiandika kwenye Instastory yake ni kweli, basi huenda kwa mara nyingine tena penzi lake na mpenzi mpya ambaye hakutaka kumtambulisha sura yake kwa wanamitandao yameporomoka tayari.

Esma aliandika ujumbe uliowaacha mashabiki wake katika njia panda akionekana kuashiria kwa asilimia kubwa kwamba huenda mambo si shwari katika huba lake.

Esma alisema kuwa mapenzi ni kama si sehemu yake, akichukulia mfano wa mtangazaji wa kipindi cha Malavidavi Wasafi FM Diva the Bawse ambaye huba lake linayumba kwa sasa hivi.

“Mapenzi yaache yaitwe mapenzi, hayachagui hayabagui. Diva tu yupo kila siku kwenye kipindi cha mapenzi [Malavidavi] na yanamliza kila siku, itakuwa sisi,” alisema.

Alidokeza kwamba huenda safari hii kosa halikuwa kutoka upande wake bali kutoka upande wa huyo mwanamume ambaye amemtema hata kabla ya kumtambulisha rasmi kwa mashemeji wa mitandaoni.

“Kuna muda unaamua kutulia mwanamume anazingua na kuna muda mwanamke… basi tafrani ila cha msingi ukipata muda wa kuenjoy mapenzi yako wewe jienjoy tu majuto baadae,” aliandika Esma.

“Sasa utasikia hata hamuendani, tuendane kwani yeye ni kiatu,” aliongeza.

Miezi ya hivi karibuni, dada huyo wa Diamond alidaiwa kuwa kwenye mahusiano na Harmonize kutokana na uhusiano mzuri ulioonekana baina yao.

Miezi minne uliopita Konde Boy alibainisha kuwa dada huyo wa hasidi wake mkuu aliweka sauti yake kwenye korasi ya wimbo wake  na DJ Seven 'Say Yes' na kumsifia sana huku aitaja sauti yake kama ya kupendeza.

 

View Comments