In Summary

•Bahati aliwataka wasanii kushikana na kuupaisha muziki wa Kenya kwenye anga za kimataifa.

Diana Marua na mumewe Bahati
Image: Instagram

Siku moja baada ya mwanamuziki Bahati Kenya kuandika ujumbe mrefu kwa wasanii wa Kenya na kulalamika kuhusu kuzembea kwao kazini na kuacha muziki wa Tanzania na Nigeria kutawala nchini, wasanii mbali mbali wameibuka na kutoa maoni yao.

Bahati katika malalamishi hayo alijitapa kuwa ndiye msanii pekee anayetegemewa kupeperusha bendera ya muziki wa humu nchini akiwataka wenzake kutomuachia kazi hiyo peke yake.

Katika kumjibu, mkewe Diana Marua ambaye pia ni rapa alisema kwamba familia yao pekee ndio inaangaliwa kwa sasa kimuziki, akisema kuwa haina shinda watashikana kitandani na pia kwenye tasnia ya muziki kuhakikisha wanainua viwango vya muziki wa Kenya.

“Itabidi mimi na wewe tushikiliane kitandani na pia tushikilie tasnia ya muziki. Nakuja kwa Amani,” Diana alisema akicheka.

Mrembo huyo mama wa watoto watatu pia aliwashauri wasanii wa Kenya kushikana na mumewe ili kuinua viwango vya muziki wa Kenya.

“On serious, wasanii wa Kenya, shikaneni mjenge industry. Huku kwa uundaji wa maudhui Team Dee ndio Top in Africa 😎 Siachilii Gear! Vinginevyo, KITATURAMBAAAA KARIBUNI SANA,” Diana Marua alisema.

Eric Omondi ambaye amekuwa akiwapiga vita wasanii wa Kenya akiwataka wazibue masikio yao na kufungua macho kuhusu mwelekeo wa muziki pia alitoa maoni yake kwa furaha akisema kuwa hatimaye juhudi zake zimeonekana kuzaa matunda.

AMKEEEENIII...WAMEANZA KUAMKA😂😂😂😂 Bro sijalala😂😂 But am happy umeona. I hope Wasanii wamekuskia. Let's take back our rightful position as LEADERS of the Region. Baraka,” Omondi alisema.

Bahati kwa kujitapa kwake alisisitiza kwamba hakuna ushindani nchini Kenya kwa sasa na kusema hiyo ni dalili mbaya sana inayoweka muziki wa kenya katika njia ya kaburini.

“Huu Ndio Wakati Wa Wanamuziki wa Kenya Kuacha Kufikiri Unaweza Kuifanya Peke Yako Na Kuja Pamoja... HAKUNA MSANII WA KENYA ANAYEWEZA KUCHUKUA muziki wetu kote ULIMWENGUNI, tunatakiwa Kufanya Kazi Pamoja kama timu ama sivyo tutaweka Curtain Raising kwa Majirani zetu... Angalia Wanachofanya na Kupitia Ushirikiano wao wa Nyumbani!” alilalama.

View Comments