In Summary

• Muigizaji huyo wa zamani wa kipindi cha Zora akiwaarifu wafuasi wake katika akuanti yake ya Instagram , alisema sasa anajivunia kuwa singo matha.

• Wawili hawa wamekuwa wakitoa vidokezo vya kila aina kwamba huenda mapenzi yao na baba wa mtoto wake wa pili, Blessing Lung’aho yalivunjika.

Jackie Matubia athibitisha kuachana na Blessing Lung'aho.

Hatimaye, Jackie Matubia amethibitisha mahusiano yake na muigizaji mwenza Blessing Lung’aho yametamatika baada ya muda wa zaidi ya miezi miwili ya kudokeza kuwa mambo huenda yakawa mabaya katika mahusiano yao.

Muigizaji huyo wa zamani wa kipindi cha Zora akiwaarifu wafuasi wake katika akuanti yake ya Instagram , alisema sasa anajivunia kuwa singo matha.

"Proud single mother of two," Jackie aliandika kwenye instastory yake.

Wawili hawa wamekuwa wakitoa vidokezo vya kila aina kwamba huenda mapenzi yao na baba wa mtoto wake wa pili, Blessing Lung’aho yalivunjika.

Matubia katika siku za hivi karibuni baada ya kukabwa koo na mashabiki ambao walitaka kujua alipo Lung’aho, amekuwa akipakia mwendelezo wa video za kuwashambulia wanaume na kuwadunisha.

Mwigizaji huyo katika klipu ambayo ameipakia kwenye YouTube yake mapema asubuhi ya Jumatano, alionekana kuashiria kabisa kwamba mwanamke ambaye anawaamini wanaume mpaka leo hii ya mwaka 2023 huenda pengine hajielewi ama amefanyiwa ulozi na uzamwamwa.

Katika mahojiano na Ankali Ray, Matubia alikwepa kujibu swali la kuwa kama wawili hao wkuw waeachana na kujibu kwa njia ya kimzaha na kuimba wimbo wa Zunchu unaoimbwa kuwa 'mali yako ishaliwa'.

Matubia amekuwa akikwepa kujibu swali la nini kilitokea au nini kinaendelea kati yake na Lung’aho kiasi kwamba hawaonekani pamoja na wala hataki kumzungumzia, ila kwa asilimia kubwa ametoa vidokezo kuwa huenda kuna ufa katika mapenzi yao.

View Comments