In Summary

• Zuchu na Diamond wamekuwa wakionesha kuchumbiana kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Mama Dangote akanusha Diamond kutoka kimapenzi na Zuchu.
Image: Screengrab//YouTube

Msanii Zuchu ameonesha tamanio kubwa la kuwa mke na kutulia kwenye ndoa.

Msanii huyo alionesha nia hii katika chapisho la muigizaji Elizabeth Lulu Instagram ambaye alikuwa amepakia picha yake, mwanawe na mumewe wakimsherehekea mwanawe siku yake ya kuzaliwa.

Lulu alimsherehekea kijana wake mdogo akiwa amemvalisha kama mwendesha magari ya mashindano, na nyingine akiwa amevalisha utepe wa medali shingoni na kushikilia mkononi taji.

Birthday Boy in JUST MK by @martinkadindaofficial shukraaani OFISHO DIZAINA 😃 (nimepost kwa heshima yako unajua” Lulu aliandika.

Moja ya maoni ambayo yalivutia watu wengi ni yale aliyoandika Zuchu akimtaka Lulu kuwamegea siri ya dua aliyoiomba hadi kumpata mume na kutulia kwenye ndoa.

Zuchu aliililia ngoa ndoa ya Lulu na mume wake Majjizo – mmiliki wa kituo cha habari cha East African TV na Radio akisema kuwa Lulu angempa hata siri tu ya dua pekee ili afe nayo akiwa kama mke wa mtu.

“Ungetuandikia tu iyo dua tufe nayo wenzio,” Zuchu aliandika.

Licha ya kutomtaja Diamond moja kwa moja, waliomjibu katika maoni hayo walihisi kabisa anahangaika kupata ndoa ya Diamond, mpenzi wake na ambaye pia ni bosi wake kimuziki katika lebo ya WCB Wasafi.

Ni hivi majuzi tu wawili hao walipoonekana kuotesha tena penzi lao baada ya kurekodiwa kisiri wakibusiana katika uwanja wa ndege.

Zuchu alimbusu Diamond kama njia ya kumpa kwaheri kabla ya kuondoka Tanzania kwenda Canada alikotarajiwa kufanya ziara ya muziki kwa siku chache.

Wawili hao wamekuwa wakizungumziwa kuwa katika mahusiano kwa Zaidi ya mwaka mmoja sasa, wakionesha viashiria vyote na wakati mwingine kukana hadharani kwamba hawako katika uhusiano wa kimapenzi bali kibiashara na kikazi.

View Comments