In Summary

• Nenga ndilo jina na lilikuwa limetengenezwa kwa herufi kubwa za kuweza kuonekana bila taabu.

• Nenga ndilo jina la kimajazi la msanii Billnass.

Nandy amuonesha mapenzi Billnass.
Image: Instagram

Nandy ametangaza mvua yake ya mawe katika mwezi ujao wa Agosti akisema kuwa utakuwa mwezi wa kuumbukwa na wengi kupitia yeye.

Msanii huyo anayefanya vizuri kwa kitengo cha wasanii wa Kike Afrika Mashariki alipakia picha na video akiwa kwenye gari lake, lakini kilichowapunga watu ni mkufu ambao alikuwa amevaa shingoni.

Nandy alionekana na mkufu ghali wenye madini tupu shingoni na kilichowaacha vinywa wazi mashabiki wake ni jina ambalo lilikuwa limetengenezwa kwa madini ya mkufu ule.

Nenga ndilo jina na lilikuwa limetengenezwa kwa herufi kubwa za kuweza kuonekana bila taabu.

Nenga ndilo jina la kimajazi la msanii Billnass.

Billnass ambaye ni mume wa Nandy alipakia video hiyo Nandy akicheza wimbo wake na Marioo na kumshukuru kwa kumuonesha mapenzi hadharani kwa kuvalia mkufu wenye jina lake, tena kubwa tu!

Billnass alisema kuwa yeye ni mbarikiwa aliyepata yote katika mtu mmoja, akisema kuwa Nandy ni Baraka kubwa ambaye pia amemzalia mtoto mwenye ulimbwende kama wake.

amani Huyu Dada ni Mzuri Jamani @officialnandy #PYG ‼️ Hv kweli una Chuma kama Hiki… Mungu akupe nini tena…jamani alaf akuzalie na Mtoto Mchunuu kama Yeye ️ “

Msanii huyo alikiri kwamba akikaa bila kutoa shukrani kwa Mungu basi atakuwa mchoyo wa fadhila, akiwashukuru vile vile wakwe zake kwa kumzalia mke kama Nandy.

“Nina Kila Sababu ya Kusema Ahsante Mungu ‼️ na Ahsante kwa Mama Mkwe na Baba Mkwe kwa kunizalia Chombo ️"”aliongeza.

View Comments