In Summary

• "Zuchu UTAMUUA BOSS WANGU” aliandika chawa wa Diamond, Baba Levo.

ZUCHU NA DIAMOND PLATNUMZ
Image: WASAFI/INSTAGRAM

Msanii Diamond kwa mara nyingine amesisitiza ubora wa Zuchu – ambaye anatajwa kuwa mpenzi wake, kuliko kutoa wimbo mpya.

Msanii huyo kupitia Instagram alipakia picha kadhaa za kuonesha mafanikio na mapokezi ya wimbo alioshirkishwa na Juma Jux, Enjoy na kusema kwamba katika muziki anadhani amemaliza kila kitu.

Diamond aliashiria kwamba katika kipindi kirefu ambacho amekaa kweney muziki, anahisi kabisa amemaliza kila kitu kwani anapofanya kit utu hupata mapokezi makubwa nadi kuhisi ni wakati wa kuacha kutoa muziki na badala yake kujikita katika kuboresha biashara yake ya mambo na vyombo vya habari – Wasafi FM na TV.

Alitoa ulinganishaji wake kati ya kutoa miziki mipya na kujifungia ndani akiwa na mpenzi wake, basi akaona kabisa kujifungia ndani na mpenzi wake ‘Chuchu’ ni bora kuliko vingine vyote.

Ndio maana sipendagi kutoa nyimbo, naonaga bora nibaki zangu busy kwenye Media… au Nijifungie zangu ndani na Chuchu,” Diamond aliandika.

Licha ya kutumia jina ‘Chuchu’ wengi waliweza kubaini kwamba alikuwa anamaanisha Zuchu lakini alifanya vile kimakusudi ili kukwepa maneno mengi yanayoweza kuibua ukakasi mitandaoni.

“Ujifungie na zuchu eti chuchu😂😂😂😂” Henry Mbike alimwambia akicheka.

“😂😂😂😂😂😂 @officialzuchu UTAMUUA BOSS WANGU” aliandika chawa wa Diamond, Baba Levo.

Diamond alionesha furaha yake kuona wimbo wa Jux ambao ameshirikishwa ukifanya vizuri, ikiwa ni chini ya wiki moja tu na tayari una watazamaji milioni tano bila video.

Awali kupitia Instastory yake alidokeza kwamba video ya wimbo huo ambayo walikuwa wametayarisha na Jux ilipotea na hivyo kuwalazimisha kuanza mipango ya kufanya video upya kuanzia Alhamisi.

 

View Comments