In Summary

• “Kwa sababu kama mimi ninafanya kazi sana. Kusema ukweli hakuna DM ya msanii tajika wa Nigeria sijaingia,” aliongeza.

Harmonize.
Image: Screengrab

Msanii wa Tanzania Harmonize kwa sasa yuko nchini Nigeria ambapo mwenyeji wake ni msanii Skales.

Katika uwepo wake nchini humo, Harmonize alitembezwa katika kituo kimoja cha radio Jumatano n alipata kufanya mahojiano ya kipekee akizungumza mengi haswa kuhusu ushindani wa muziki wa Afrika mashariki dhidi ya ule wa muziki wa Afrika Magharibi.

Katika kipande kifupi cha mazungumzo hayo ambacho kimepatikana, Harmonize alisikika akikiri kwamba muziki wa Afrika Magharibi haswa mataifa ya Nigeria na Ghana umekwenda mbali sana katika kupiga hatua kimataifa ikilinganishwa na muziki wa Afrika MashariKI.

Msanii huyo alitoa changamoto kwa wasanii wenzake wa Tanzania kushikana pamoja ili kuusukuma muziki wao mbele kwa pamoja, akisema kwa upande wake amejaribu sana mpaka kuingia kwa DM za wasanii mastaa karibia wote kutoka Nigeria.

“Nazungmzia kuhusu muziki wa Tanzania, unaona kama sasa ukiangalia tunajaribu lakini bado sana hatujafika ukitulinganisha na Nigeria kimuziki. Kwa hiyo hakuna haja ya kujionesha na ushindani wa ni nani ndiye nani mwenye talanta kubwa. Nafikiri ni muda wa kuungana na kujifunza kutoka kwa ndugu zetu wa Nigeria na Ghana kama njia moja ya kusukuma mbele tamaduni yetu ya muziki,” Harmonize alisema.

“Kwa sababu kama mimi ninafanya kazi sana. Kusema ukweli hakuna DM ya msanii tajika wa Nigeria sijaingia,” aliongeza.

Harmonize anazidi kutamba na kutambaa kote duniani kwa goma lake la Single Again ambalo katika kipindi hicho liliwatoa watangazaji kijasho wakati wa kusakata densi, mtangazaji huyo akimwambia kwamba katika wimbo huo alitengeneza jitu la wimbo.

 

 

View Comments