In Summary

• Leonard Mambo Mbotela kwa sasa amestaafu baada ya kufanya kazi katika shirika la habari la serikali ya Kenya, KBC kwa Zaidi ya miongo minne.

Leonard Mambo Mbotela na Gidi wa Radio Jambo.
Image: FACEBOOK

Mtangazaji wa stesheni ya Radio Jambo Gidi Ogidi amefunguka kwamba katika taaluma yake ya utangazaji kwa miaka 16, siku zote amekuwa akitamani kama kungekuwa na uwezo wa kurudisha muda nyuma na apewe nafasi ya kuchagua mtangazaji wa kufanay kazi naye basi angemchagua mtangazaji mkongwe wa VOK, Leonard Mambo Mbotela.

Gidi alipakia picha kwenye Facebook yake wakiwa na mkongwe huyo wa utangazaji wakiwa wamefurahia kwa kicheko na kusema kwamba angefurahi sana kufanya kazi naye ingekuwa ni uwezo wa kurudisha muda nyuma angalau kidogo tu.

“Nimefanya utangazaji wa redio kwa miaka 16, lakini ikiwa ningepewa nafasi ya kushikanishwa na mtu wa redio, nitamchagua gwiji Leonard Mambo Mbotela,” Gidi alisema.

Leonard Mambo Mbotela na Gidi

Hata hivyo, Gidi hakumpuuza mtangazaji mwenza Ghost ambaye wamekuwa wakifanya kazi naye kwa miaka kadhaa kwenye Radio Jambo awamu ya Asubuhi na kusema kwamba wangeungana na Mbotela ingekuwa ni timu moja hatari sana ya kuteka mawimbi ya utangazaji nchini.

“Hebu fikiria Mbotela, Gidi na Ghost Asubuhi? Vicheko baada ya vicheko…Tunasherehekea kwa fahari lejendari Leonard Mambo Mbotela,” aliongeza.

Mbotela na watangazaji wa Radio Jambo
Image: Facebook

Leonard Mambo Mbotela kwa sasa amestaafu baada ya kufanya kazi katika shirika la habari la serikali ya Kenya, KBC kwa Zaidi ya miongo minne.

Wengi wanamkumbuka mtangazaji huyo kwa kipindi chake cha muda mrefu ‘Je huu ni uungwana’ ambacho kimekuwa kikipeperushwa kwenye kituo hicho cha redio majira ya asubuhi, akizungumzia kuhusu vitendo vya kuudhi ambavyo Watu hufanya kwa wenzao.

 

View Comments