In Summary

• Wengine walisema kwa mara ya pili Diana amefaulu kumtoa Bahati kwenye muziki kwenda kwa uanablogu.

• Kwani mara ya kwanza wanahisi ndiye alichangia kumhamisha msanii huyo kutoka Injili hadi sekula.

Diana na Bahati.
Image: Instagram,

Familia ya Bahati na mkewe Diana Marua katika siku za hivi karibuni wamewafurahisha mashabiki wao katika skits za kuchekesha ambazo wamekuwa wakifanya na kupakia katika mitandao yao ya kijamii.

Licha ya wengine kusema kwamba Diana amefanikiwa kumtoa Bahati katika muziki na kumhamishia katika kukuza maidhui, lakini kuna wengine ambao wamefurahia jinsi wawili hao wamekuwa wakikuja na video fupi fupi za kuchekesha, ambazo haswa huzingatia katika maisha ya kawaida ya kila siku kwenye ndoa.

Wanandoa hao wamepakia klipu fupi ikionesha jinsi mwanamke anakuwa katika ndoa wakati wamegombana na mumewe.

Katika klipu hiyo fupi, Diana aliandika kwamba ni matukio yanayomkuta mume wakati wamegombana na mumewe na kuingia kitandani kulala akifikiria ugmvi na mkewe umeisha – kumbe mke bado amebeba kinyongo moyoni na ana njama ya kulipiza baada ya mumewe kulala.

Bahati alikuwa amelala na kujibukia blanketi kutoka kichwani hadi mguuni, lakini aliamua kubadilisha sehemu ya kuweka kichwa akaweka miguu.

Diana kwa haraka alinyata kwenye chumba hicho na kuchukua mto wa kulalia, akiwa na nia ya kumnyonga mumewe Bahati.

Kama ilivyo kawaida ya kulala kwao, alikuwa na uhakika kwamba kichwa cha mumewe kipo sehemu ile ya kawaida na kwa haraka akafinya kwa kumnyonga, akidhania amepaka shingo barabara.

Asichokijua ni kwamba Bahati alikuwa amebadilisha na kuweka miguu sehemu ya kichwa, na hivyo Diana alizidisha nguvu zake katika kufinya akiwa na uhakika ni kichwa ananyonga.

Bahati kwa ghafla aliamsha kichwa kutoka upande wa pili wa kitanda na kumfumania mkewe akiwa katika harakati ya kumnyonga miguu – akiamini ni kichwa – na kumuuliza, “unafanya nini?”

Diana, kama mwanamke yeyote asiyeishiwa na cha kujitetea nacho, alijibu kwa haraka kwamba alikuwa anajaribu kumkanda mumewe miguuni, akijichanganya kwa maneno.

“Nilikuwa nakukanda mguu, nakukanda. Nakupanga. Nakupanga. Nakupanga na hupangiki,” Diana alimjibu kwa uso usio na mzaha kabla ya kuondoka katika chumba hicho.

Mashabiki wao walifurahia klipu hiyo ya kuchekesha na kumpongeza Marua kwa jinsi alivyoigiza utadhani ni tukio la kweli kumbe ni mzaha tu.

Wengine walisema kwa mara ya pili Diana amefaulu kumtoa Bahati kwenye muziki kwenda kwa uanablogu, kwani mara ya kwanza wanahisi ndiye alichangia kumhamisha msanii huyo kutoka Injili hadi sekula.

View Comments