In Summary

• Katika mashambulizi hayo, Diamond alimwambia Alikiba kwamba tatizo lake mpaka kupitwa na wasanii wachanga ni kukubali kuandikiwa mistari ya miziki zake.

Diamond na Alikiba watandikana ngumi
Image: INSTAGRAM

Diamond amemtambia mshindani wake wa muda mrefu katika muziki wa Bongo Fleva Alikiba akisema kwamba hata mtoto wa juzi kwenye muziki, Zuchu amemshinda kushindana naye.

Kupitia insta story yake, Diamond alipakia kiunganisho cha ngoma mpya ya Zuchu kwenda YouTube, Honey na kuonesha kwamba ngoma hiyo ambayo imetoka mwishoni mwa juma ilikuwa ndio gumzo Tanzania na ilikuwa imeshikilia nambari moja YouTube kwa trending.

Diamond aliandika maneno ya kumshambulia Alikiba akisema kwamba hafai kumpigia kelele kuhusu kuchukua baadhi ya beat za ngoma za wasanii wa Nigeria wakati yeye amepitwa hadi Zuchu, msanii ambaye hana miaka mingi kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Katika mashambulizi hayo, Diamond alimwambia Alikiba kwamba tatizo lake mpaka kupitwa na wasanii wachanga ni kukubali kuandikiwa mistari ya miziki zake.

Diamond aliwambia kwamba amezidi katika kukubali kuandiiwa akisema kuwa watu huwa wanapenda mashairi anayojitungia mwenyewe na wala si yale ya kutungiwa.

Diamond alimsifia Zuchu akisema kwamba ameshikilia nambari moja YouTube hata bila kufanya promo yoyote kwa ngoma hiyo ya Honey.

“Dah, yaani hata baada ya kuorodhesha mitihani lakini bado mmepigwa tena na Zuchu, halafu katoto ka watu hakajafanya interviews wala hata party... tatizo wewe mfalme [Alikiba] wewe nawe umezidi sana kuandikiwa siku hizi… ungejitungia mwenyewe zako tu kama unavyojitungia, mbona watu wanapenda vile tu,” Diamond aliwambia Alikiba.

Alimalizia kwa kumwambia Alikiba kwamba kwa vile ameshindwa kushindana naye na pia kupitwa hata na vitoto vichanga katika muziki, akae kando na ‘Sumu’ yake ili kujifurahisha na ‘Enjoy’ na ‘Honey’ akimaanisha ngoma yake na Jux pamoja na hiyo mpya ya Zuchu.

Alikiba na Diamond wamekuwa wakishambuliana katika sehemu kubwa ya mwezi huu wa Julai baada ya Diamond kulichangamsha genge kwa madai kwamba Juali mpaka Januari mwakani hamuachii mtu nambari moja kwenye trends.

Kauli hii ilikuja kama filimbi ya kumuamsha wasanii wa bongo kutoka usingizi mzito ambapo kila mmoja amechangamka katika kiachia ‘mvua yake ya mawe’ ili kufifisha azma ya Diamond kushikilia namba moja kwenye trends kwa miezi hiyo sita.

 

View Comments