In Summary

• Hata hivyo, msanii huyo pia alisema kuwa yuko radhi kukubali kutopata mtoto na Musila,

Image: INSTAGRAM// ESTHER MUSILA

Kwa mara nyingine tena msanii wa injili Guardian Angel amelivalia njuga suala la kupata mtoto na mkewe Esther Musila mwenye umri wa miaka 52.

Katika mahojiano na chaneli ya 2mbili, mwanablogu hakuchoka tena kumuuliza kuhusu uwezekano wake kupata mtoto na mkewe ambaye kisayansi anasemekana hatoweza kuzaa tena kutokana na umri wake.

Angel alisema kwamba kikubwa wanachokizingatia kwa sasa ni kuishi kwa furaha na Amani hadi kushibana wenyewe kwa wenyewe lakini pia akasema kuwa atamshukuru Mungu sana endapo atampa mtoto na Esther Musila.

Hata hivyo, msanii huyo pia alisema kuwa yuko radhi kukubali kutopata mtoto na Musila, akionekana kukubaiana na dhana kwamba huenda haitotokea kwani Musila ameshapita umri wa miaka 45 – ambao wanasayansi wanasema ndio umri wa mwisho kwa mwanamke kupata mimba.

"Uzuri zaidi kuhusu ndoa yangu ni napenda kuwa kwenye ndoa yangu, napenda sana kumpenda mke wangu, ana maana zaidi kwangu kuliko kunipa watoto. Nikipata nafasi ya kuzaa na mke wangu, nitamshukuru sana Mungu lakini pia isipotokea ni sawa," alisema.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 33 pia alipata kuzungumzia uhusiano wake na watoto wa Musila amabo wengi wanasema ndio rika lake akisema kwamba wanamheshimu na kusema kwamba watoto hao watatu wa Musila ni sehemu ya maisha yake.

Guardian Angel pia alisema kwamba kuna watu wengine walipata watoto lakini wakakosa furaha katika ndoa, akisema kwamba yeye ana Amani kwenye ndoa na iwapo atapata watoto basi itakuwa kama nyongeza kwa ndoa iliyotimia.

“Kwangu mimi nina watoto ambao ninawalea, nina watoto ambao nimewapeleka shule na Mke wangu ana watoto ambao ni sehemu ya maisha yangu, kuna watu wamepata fursa ya kuolewa na kupata watoto, lakini hawana furaha katika mahusiano yao,” alisema.

Kwa mara kadhaa wanandoa hao wamekuwa wakijibu kwa ukali maswali kuhusu kupata watoto na kipindi kimoja Angel aliwakemea wanaume wanaomuuliza ni lini atapata watoto akisema kwamba hata hawajui pengine watoto wanaolea majumbani mwao ni wake.

View Comments