In Summary

• “Mambo ya watu mitandaoni hayatuathiri hata kidogo. Sisi tunafurahia maisha, sisi tunaishi maisha yetu mazuri Zaidi" - Guardian.

Image: Instagram

Msanii wa injili Guardian Angel amefutilia mbali uwezekano wa ndoa yake na Esther Musila kuvunjika akisema kwamba wanashibana na wanaishi maisha ya furaha ya kilele.

Angel alisema katika mahojiano na chaneli ya 2Mbili kwamba ndoa yao imejengwa katika misingi ya Mungu na haiwezi kusambaratika kwani Mungu ndio alipanga wakakutana vile walikutana japo kumekuwa na makombora mazito dhidi yao kwa kigezo cha utotafauti mkubwa kiumri.

“Kulikuwa na dhihaka nyingi dhidi yangu wakati nilioa. Hao watu wako wapi sasa hivi? Kwa sababu kila mtu anataka kuangalia maisha jinsi amezoea kawaida. Mimi nimeweza kufanikiwa katika ndoa yangu na naamini watu wamenza kuwa na maoni tofauti kuhusu ndoa yangu,” Angel alisema.

“Mambo ya watu mitandaoni hayatuathiri hata kidogo. Sisi tunafurahia maisha, sisi tunaishi maisha yetu mazuri Zaidi na mke wangu, tunaroll tunabowl, yaani sisi tuko kilele, unaelewa,” aliongeza.

Guardian Angel pia alisema hakuna haja ya kushinikizwa na mtu yeyote kuoa mwanamke wa rika lake akisema kwamba wengi ambao wameoa wanawake wa rika lao wengi wapo huku nje wanachepuka.

“Asilimia kubwa ya watu ambao wako katika uhusiano mchanga wanachepuka, wanahisi kuna mtu mwingine ambaye ni wa maana, kwa hiyo kuna umuhimu gani wa kuwa katika uhusiano wa aina hiyo. Ndio una watoto, umeoana na mtu wa rika lako lakini bado hata huyu mtu wa rika lako tena unatamani mwingine wa nje. Haina umuhimu. Kuna mengi kwa ndoa kuliko hata watoto,” Angel alisema.

View Comments