In Summary

• Msanii huyo kwa sasa yuko nchini Ujerumani kwa ziara ya muziki wa mugithi na ameendelea kujitambua kama Babake Nimu.

Image: FACEBOOK.

Afisa wa polisi ambaye pia ni msanii pendwa wa Mugithi Samidoh yuko nchini Ujerumani kwa ziara yake ya muziki barani Ulaya.

Msanii huyo ameendelea kuwapunga mashabiki wake kwa misemo na kauli ambazo anachapisha kwenye kurasa zake za mitandaoni.

Ya hivi karibuni imekuwa kauli inayofuma upande wa wanaume akisema kwamba sumu ambayo ni tamu kwao ni mwanamke mzuri na pombe iliyokolea pekee.

“Mvinyo mzuri wa mitende na mke mzuri ni sumu mbili tamu kwa mwanaume,” Samidoh alisema.

Msanii huyo katika ziara yake ya Ujerumani, alionekana akitumbuiza katika shoo mjini Frankfurt na tayari ametangaza shoo nyingine nchini Australia mwezi Septemba.

Samidoh ambaye amekuwa akigonga vichwa vya habari katika miaka ya hivi karibuni kutokana na migogoro ya kimapenzi baina yake na babymama wake wawili – Edday Nderitu na Karen Nyamu, mwishoni mwa juma alitoa tamko ambalo lilionekana kutupa kijembe kwa mke wa kwanza Edday Nderitu.

Samidoh aliandika kwamba mtu yeyote anayekwenda kwa hadhara na kukuzomea huko badala ya kukufuata faraghani kukuambia suala lake si mkweli bali anatafuta kusikilizwa tu.

Tamko hili lilitafsiriwa na wengi kama kijembe kwa Edday aliyechapisha ujumbe mrefu akisema kwamba msanii huyo hajawahi msaidia katika malezi na matunzo ya watoto.

Edday, katika kile alisema ni kunyoosha maelezo, alisema alichukua uamuzi wa kumuacha Samidoh ilia pate kujivinjari na mwanamke ambaye alikuwa na haja naye.

Mama huyo wa watoto watatu ambaye sasa yuko nchini Marekani na wanawe alisema hatua ya kwenda na wanawe ni kumlinda kisaikolojia binti yake wa kwanza ambaye ni tineja dhidi ya athari zinazotokana na mgogoro wa kimapenzi unaowahusisha wazazi wake na Karen Nyamu.

 

View Comments