In Summary

• Mzozo huo kwenye mitandao umeibua hisia mseto kwa mashabiki, ambapo baadhi wanadai kuwa Diamond alinawiri chini ya Alikiba na hivyo anapaswa kumheshimu.


Diamond aonesha kuchukizwa na kulinganishwa na wasanii duni.
Image: Facebook

Mwanamuziki Diamond Platnumz amedakia kuwa Alikiba si mtu wa kulinganishwa naye katika sanaa ya muziki kwani yupo nyuma sana wa kulinganishwa.

Katika mzozo unaoibua hisia mseto miongoni mwa wanamitandao, msanii huyo wa bongofleva ameeleza kuwa amepiga hatua kubwa kwenye muziki licha ya kumpata Alikiba katika sanaa hiyo.

Malkia wewe umewekeza kwenye uzalishaji upi wakati video yangu moja ni sawa na video zako 20, wimbo wangu mmoja ni sawa na nyimbo zako 20! Tatizo ulilo nalo ni kuwa hakuambii ukweli wanakudanganya na ndio maana nimekupata kwenye muziki miaka ishirini na nikakupita,” Simba alimfokea mwenzake Kiba katika ukurasa wake wa Instagram.

Gwiji huyo wa muziki Tanzania aidha aliendelea kujipiga kifua kuwa hali ya juu ya muziki wake ndiyo imemfanya kumpiku Alikiba kwa kila kitu katika mitandao kuhusu sanaa ya muziki na midundo kwa ujumla.

Nimekupita kila kitu; kimauzo, kituzo, wafuasi, sabskriba, watazamaji, wasikilizaji, bei katika shoo, kimaendeleo au kiufupi tuseme kila siku,” aliposti Diamond Platnumz.

Katika maandishi hayo, Simba alijidai kuwa yeye pia hufanya shoo zake na zikawa nzuri zaidi ndani na nje ya mko wa Afrika Mashiriki, ikilinganishwa na mwenzake aliyesema kuwa hajawahi kutoka nje ya Afrika Mashariki kufanya shoo zake.

Miaka karibia ishirini kwenye muziki hadi leo umeishia kufanya shoo katika eneo la Afrika Mashariki! Tena eneo hilo la Afrika Mashariki kuna nchi hujaenda kufanya shoo,” aliendelea kumfokea.

Alikiba maarufu Kingkiba, alijibu shutuma kwa Simba na kusema kuwa ajifunze sauti ambapo kwa kujibu shambulizi hilo, Diamond Platnumz alikiri kuwa wanao na uwezo na ujuzi mzuri wa sauti ni Burnaboy au Davido pekee na kwa hivyo iwapo ni kujifunza atajifunza kutoka kwao.

Mzozo huo wa mitandaoni umeibua hisia mseto kwa mashabiki, ambapo baadhi wamedai kuwa Diamond alinawiri mikononi mwa Alikiba, na hivyo anapaswa kumheshimu na wala si kumshutumu kila uchao.

View Comments