In Summary

• Naamini Upendo umetawala sana Mioyoni mwenu japo kuwa sometimes Mambo ya ridhki ndo yanafanya kuwa kuna namna tofauti But NOTHING SERIOUS - Marioo.

Diamond Platnumz, Al8ikiba
Image: INSTAGRAM

Saa chache baada ya wasanii Alikiba na Diamond kuvuana nguo hadharani mitandaoni kwa maneno ya chache, video imeibuka ikiuonesha msanii Diamond akipagawa kwa densi ya wimbo mpya wa Alikiba, Sumu.

Video hiyo inawaonyesha Diamond akiwa na mdogo wake na Alikiba Abdu kiba, Juma Jux, Mbosso miongoni mwa watu wengine kwenye maeneo kama ya tafrija hivi na walikuwa wanafurahia wimbo huo wa Sumu ambao Alikiba amemshirikisha Marioo.

Video hiyo imepakiwa kwenye Instagram na Marioo na imewaacha wengi bila maneno vinywani.

Marioo alipakia video hiyo na kusema kwamba binafsi yeye anawakubali Diamond na Alikiba kwa kuwa wao ndio sababu ya uwepo wake kwenye muziki.

Aidha, msanii huyo alidokeza kwamba huenda kile ambacho kinaonekana mitandaoni kuwa ni ugomvi baina ya wasanii hao wawili huenda sivyo katika hali halisi.

Alisema kwamba ni uchachu tu wa kuchangamsha genge ili kusukuma muziki wa Bongo Fleva mbele wala hakuna kikubwa kinachoendelea baina yao kama ugomvi wa kutoonana ana kwa ana.

Binafsi Nawapenda na Kuwaheshimu Brothers wote kwasababu Nyie ndo sababu ya Nafasi yangu ️‍🔥Naamini Upendo umetawala sana Mioyoni mwenu japo kuwa sometimes Mambo ya ridhki ndo yanafanya kuwa kuna namna tofauti But NOTHING SERIOUS 🧐 Let's Take bongofleva to the Top,” Marioo aliandika. 

Video hiyo imeonekana kuchukua mkondo tofauti kabisa wa kimawazo kwa wale ambao walikuwa wanadhani kwamba Diamond na Alikiba ni maadui wa kuvuana nguo mitandaoni.

Wengine wanahisi ni moja ya kiki iliyokwenda skuli ambayo wasanii hao wanajaribu kutumia fursa ya dhana ya ugomvi kati yao ili kuupaisha muziki wa Bongo kwenda mbele.

Na kweli kama ni kiki basi wamefanikiwa sana, kwani kushambuliana kwao mitandaoni kumewafanya kutrend sit u nchini Tanzania bali Kenya pia ambako wana ufuasi mkubwa kwa muda mrefu.

Swali ambalo wengi wanajiuliza ni je, inawezekana Diamond kumtukana Alikiba kwa kumuita Malkia na hata kumwambia kwamba hana lolote katika kujiita vocalist na wakati huo huo kuonekana kufurahia utunzi wake wa muziki?

 

View Comments