In Summary

• "Mimi ninaamini nyota lakini mbona usinioneshe? Watu wanajua kucheza na saokolojia yako mpaka uibiwe na uitike,” Mgogo alisema.

Mchungaji ashauri wanaume kuwapa wake zao nafasi ya kupiga kelele.
Image: facebook

Mchungaji wa Tanzania Daniel Mgogo amewasuta baadhi ya waumini ambao wanakubali kudanganywa na waumini bandia kuhusu kuombewa kupata baraza za kufunguka kwa mitikasi yao.

Akihubiri katika kanisa la Deliverance Church Springfield jijini Nairobi, Mgogo alisema kwamab waumini wengi wana akili nyingi lakini anashindwa ni kwa nini wanakubali kuoshwa na kubebewa akili na maneno ya wachungaji.

Mchungaji huyo aliwatahadharisha watu dhidi ya baraza za kuombewa ili zije kwa haraka na kwamba baraza za aina hiyo si za kweli na huyeyuka vile vile.

“Baraka zinazochipuka kwa haraka na zenyewe uwe na mashaka nazo, huenda zikakuondoa duniani. Kuna watu wanasema eti tutakuombea uwe na biashara kubwa, mwambie ngoja kwanza nianze na ya machungwa, namna ya kurudisha change nijifunze ndio nianze kupokea makontena kutoka China,” Mgogo alishauri.

“Yaani wewe unataka upokee makontena kutoka China hali ya kuwa hujawahi kumiliki hata kakibanda. Mara ‘nataka Bwana anipe gari kubwa’, utaweka nani mle? Magari hayatembelei maji. Mungu atakupa msingi kwanza ili hata akikupa gari, uwe na uwezo wa kuweka mafuta usitusumbue kwamba gari limezimikia kwa njia,” Mgogo aliongeza.

Hata hivyo, mchungaji huyo hakufutilia mbali Imani katika nyota lakini akawaambia waumini kabla ya kukubali kutoa hela kwa ajili ya ‘kuombewa kupata nyota’ wanafaa kutathmini wenyewe na kuchanganua kwa akili walizo nazo.

“Mchungaji asikuje kukudanganya eti ameona nyota yako mahali na anataka utoe laki moja ili akurudishie, unakwama wapi mbona una akili nyingi? Mimi ninaamini nyota lakini mbona usinioneshe? Watu wanajua kucheza na saokolojia yako mpaka uibiwe na uitike,” Mgogo alisema.

 

View Comments