In Summary

• Wengine walimwambia kwamba ugomvi huo haumhusi na badala yake kumtaka kupambana na wanawake wenzake kimuziki kama Nandy.

Harmonize na Kajala
Image: Instagram

Msanii wa WCB Wasafi, Zuchu naye ameonekana kujitosa katika ugomvi wa Harmonize na aliyekuwa mpenzi wake Kajala pamoja na binti yake.

Zuchu kupitia Instagram alichapisha picha za skrini akionesha ufanisi mkubwa ambao ngoma yake mpya ya Honey inazidi kumzolea, na kusema kwamba kwa sasa ndiye namba moja kwenye YouTube kupitia ngoma hiyo.

“BADO NAMBA 1 🙌🙌🙌🙌 Usifungue kwenda mbele bana,” Zuchu alionya kwa utani kama njia ya kuwachochea watu kutaka kuona anachowakataza wasikione.

Katika picha hizo, mwisho aliweka video Fulani ya mtu ambaye alikuwa anaigiza kama Harmonize huku mwingine akionekana kama mwanahabari na kumkimbilia nyuma ya kipaza sauti akimuuliza kitu.

Mtu huyo anayeigiza kama Harmonize anageuka na kumjibu huku akiweka kile kilichoonekana kana ni jiti la sigrara mdomoni kabla ya kuondoka.

Mashabiki wa Zuchu walioona video hiyo walihisi naye ni kama anamchokoza Harmonize, wengine hadi wakimtahadharisha vikali kwamba anakokwenda kukanyaga si kuzuri kwani Harmonize atamparura.

Wengine walimwambia kwamba ugomvi huo haumhusi na badala yake kumtaka kupambana na wanawake wenzake kimuziki kama Nandy.

“Na wewe unataka kudandia gari kwa mbele dogo jitambue umemshindwa Nandy huku ndo utazama” Sheby Clever alimwambia

“Itakuwa anataka mushedede wa kimakonde maana wa domo haumtoshi kwhy utapata tu, mtoto akililia wembe mpe na pia mtoto akililia dudu basi mpe pia apate mimba” Bangu Frank.

“Team zuchu please tuandae makombora... harmonize si mrahisi venye tunafikiria” Faithster.

“Utaweza ligi ya konde kama fantana nusu akuue” mwingine alimwambia.

“Last slide 😂😂 ngoja konde akunywee pombe na wewe ashushe waraka wa yakobo juu yako 😂😂😂” mwingine alimtahadharisha.

 

View Comments