In Summary
  • MC wa Ikulu ameshiriki picha kwenye akaunti yake rasmi ya mtandao wa kijamii na kuwafahamisha Wakenya kuhusu afya yake.

Vincent Mwasia Mutua, maarufu kwa jina la kisanii Chipukeezy, Mchekeshaji maarufu wa Kenya na Mc wa Ikulu amevunja ukimya siku chache baada ya kulazwa katika Hospitali ya Nairobi West kutokana na ugonjwa ambao haujajulikana.

MC wa Ikulu ameshiriki picha kwenye akaunti yake rasmi ya mtandao wa kijamii na kuwafahamisha Wakenya kuhusu afya yake.

Katika picha Chipukeezy alionekana dhaifu kidogo. Hata hivyo amewahakikishia Wakenya kwamba anaendelea kupata nafuu.

"Katika safari ya maisha, afya ni hazina kuu. Ninaendelea vyema katika kupona kwangu na tunamshukuru Mungu" aliandika Chipukeezy kwenye akaunti zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Mchekeshaji huyo alitoa habari hizo njema kwenye mtandao wake rasmi wa kijamii wa Instagram akiwahakikishia mashabiki wake kuwa anaendelea vizuri na kwamba ameruhusiwa kutoka Hospitali.

Alipigwa picha akitumia muda katika moja ya mashamba yake.

Haya yanajiri siku chache baada ya kulazwa hospitalini. Dennis Itumbi, mmoja wa washirika wake wa karibu alikuwa amefichua kuwa Chipukeezy alikuwa na matatizo ya kiafya ambayo yalikuwa bado yanafanyiwa majaribio wakati huo na hivyo kusababisha kulazwa hospitalini.

Chipukeezy alikuwa na onyesho kubwa lililokusudiwa kufanywa tarehe 5 Agosti na ambalo lingehudhuriwa na watu mashuhuri akiwemo binti wa kwanza Charlene Ruto.

Hata hivyo iliahirishwa kutokana na suala la Afya.

Mashabiki walimtakia afueni ya haraka na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

tomdaktari: Itakua sawa

timo: Quick recovery kasee @chipukeezy

thepositivethinker: It will be well Bro, Solidier on.....

lilian: Get well soon Chipu.

washington: quick recovery

edwin: Quick recovery mzee Chipuuu 🙏

 

View Comments