In Summary

• Fatxo alisema kwamba Mungu ni rafiki wake wa kibinafsi na kujua hilo kulimpa msukumo wa aina yake kujua kwamba hakuna cha kushindikana.

DJ FATXO

Msanii wa Mugithi DJ Fatxo amerejea nchini baada ya wiki kadhaa kwenye ziara ya muziki nchini Uingereza.

Msanii huyo akizungumza katika uwanja wa ndege wa JKIA wikendi iliyopita baada ya kutua, alisema kwamba baada ya siku kadhaa za kukumbana na tuhuma za kuhusishwa kwenye sakata la kifo cha rafiki yake Jeff Mwathi, alihitaji muda wa kwenda mbali kidogo ili kujipanga upya na kujikung’uta mavumbi.

Fatxo alisema kwamba alichojifunza akiwa huko mbali katika mataifa ya watu ni kwamba hakuna kitu cha maana katika maisha kama kuwa na uhuru, mtu ukiwa unajua hakuna kesi inayokuandama.

“Lakini kitu ambacho ninaweza sema ni kwamba hakuna kitu cha maana kama kuwa na uhuru. Namshukuru Mungu kwa kuondolewa tuhuma, namshukuru Mungu kwa kuachiliwa huru, na hakuna kitu kizuri kama hicho. Hakuna mtu mwingine naweza mshukuru isipokuwa Mungu,” Fatxo alisema.

Msani huyo alisisitiza kwamba hana uhamsama na mtu yeyote wakiwemo wale ambao walikuwa wanaendeleza haraakti mitandaoni za kutaka atiwe hatiani kwa kumhusisha na kifo cha aliyekuwa rafiki yake Jeff Mwathi.

“Mimi tayari nimewasamehe. Unajua kama ukiangalia mtu kama Yesu, alikuwa anaenda na kufanya miujiza na bado watu walimchukia, mimi sio wa kwanza. Nimesamehe kila mtu, nyinyi ndio mko na ubaya na mimi, mimi sina ubaya na mtu na hivyo ndivyo nimekuwa nikifanya. Mimi ni mtu wa kusamehe na huwa ninaachilia kitu kitu kwenda na kumkaribisha Mungu,” alisema.

Fatxo alisema kwamba Mungu ni rafiki wake wa kibinafsi na kujua hilo kulimpa msukumo wa aina yake kujua kwamba hakuna cha kushindikana.

“Katika sakata hili ote nilijifunza kwamba watu pekee ambao unafaa kuwaweka karibu na wewe ni familia yako tu. Familia haiwezi kutenga. Pia unafaa kuwa makini wakati wa kuchagua marafiki, wengi wa marafiki zangu walinitoroka wakati niliwahitaji,” alisema.

 

View Comments