In Summary
  • Wimbo wa Kiswahili unamsifu Ngesh wa Vasha kama mwanamke anayetamanika zaidi kwake.
Pritty Vishy sasa anataka kurejea katika mahusiano na Stevo Simple Boy
Image: Instagram

Rapa Stevo Simple Boy amekiri kuwa anampenda sana rapa Ngesh aliyejizolea  umaarufu kwa wimbo wa Kaveve Kazoze.

Stevo alienda kwenye ukurasa wake wa TikTok kufunguka kuhusu hisia zake akisema kwamba anataka Ngesh awe mchumba wake.

“Yoh, huyu ni Stevo Simple Boy Mondi wa Kenya manze kuna mwanadada pale naona amenivutia sana anaitwa Kaveve Kazoze(Ngesh). Kama ako single mwambie Stevo Simple Boy mzee wa matulenga namtamani mfikishie ripoti mwambie Stevo Simple Boy nimedata kwake lazizi wangu habi kwake sitamsuta nitakuwa naye na mambo itakuwa freshi aje awe mchumba wangu,” rapper huyo alisema.

Video hiyo tangu wakati huo iliibua hisia tofauti kutoka kwa mashabiki, wengine wakimtaka azingatie kutafuta pesa kwanza kabla ya kujihusisha na maswala ya mapenzi.

Anapiga busu kwenye kamera huku akimhakikishia upendo wake wa dhati.

Alishiriki kipande cha wimbo maalum kwa Ngesh ambapo anasema urembo wake umemponza, na yuko tayari kulewa kwa mapenzi naye.

Anatumia emoji nyingi nyekundu za moyo kama nukuu yake ya uwekaji wakfu wa wimbo ikiwa ni pamoja na picha ya wakati Ngesh alipofanyiwa urembo na wigi nzuri ya pembeni na lipstick.

"Waseme nini kwako siwezi banduka na fahamu zangu umezifunika," mstari wa kwanza wa wimbo unaenda.

Wimbo wa Kiswahili unamsifu Ngesh wa Vasha kama mwanamke anayetamanika zaidi kwake.

"Nimekamatika, mapenzi kama ya cooker, hata waseme nini huko siwezi banduka, lakini nahamu zangu umezifunika. Tamtam, mapenzi tamtam, Ukiniita simple, mapema na come come, faster, mpeni nishampata, sina wasi wasi,"

 

 

 

 

 

View Comments