In Summary

• Mwijaku alisema kwamba Harmonize anakosea kuwaumbua Kajala na binti yake na anafaa kufahamu kwamba hata yeye ana binti na hawezi jua kesho yake na malipo ni hapa hapa duniani.

Mwijaku awashauri Harmonize na Kajala
Image: Instagram

Mtangazaji mbwatukaji Mwijaku amemshauri Harmonize kukoma kumuumbua Kajala pamoja na bintiye kwa yale amabyo aliwafanyia kipindi ni mpenzi wa Kajala.

Mwijaku alisema kwamba Harmonzie anaonesha kutokomaa kiakili kwa kujaribu kumuingiza binti Paula kwenye ugomvi wao yeye na Kajala na kujichuna sikio kukumbuka kwamba malipo ni hapa hapa duniani kwani hata yeye ana mtoto wa kike pia na hawezi jua kesho yake.

“Harmonize hata kama wewe ndio ulikuwa mtu wa kwanza kuzungumza naye [Paula] hufai kuja kutumabia. Msitiri mtu, sisi kwa Imani ukimsitiri binadamu mwenzio Mungu atakuja kukusitiri. Mimi nikuombe umsitiri Paula, bado ni binti mdogo sana. Inawezekana alifanya kwa utoto na ujinga kutofahamu, msitiri. Usimuingize kwenye vitu ambavyo utaharibu future yake,” Mwijaku alimuomba Harmonize.

“Hivi vinavyokuja mkiendelea hivyo hatujengi, tunabomoa, kumbuka nawe una mtoto wa kike, nikwambie malipo ni hapa hapa duniani, kwa Mungu ni mahesabu tu,” aliongeza.

Mwijaku ambaye ndio alikuwa mtu wa kwanza mwaka jana kudai kwamba Harmonize alikuwa anatoka kimapenzi na mama na binti yake alisema kwamba baada ya sakata la kupapurana mitandaoni na Harmonize, alifanya maongezi na Kajala na kumtaka kukoma kujibu kila kitu.

“Mimi leo nimeongea na Kajala nikamuambia stop this. Acha kujibu kila kitu. Hakuna binadamu anapewa kitu kwa kujibu kila kitu. Huyo bwana atakughasi utaongea kila kitu na kuna vitu utashindwa kuvisema. Kaa kimya, ukikaa kimya ni fimbo. Mimi nikisema kitu halafu wewe usinijibu najiona mwehu, chizi,” Mwijaku alisema.

Mwijaku alisema kinachoendelea baina ya Harmonize na Kajala si wivu wa kimapenzi bali ni kutokomaa kabisa.

“Wote wawili kwenye masuala ya mapenzi hawajakomaa. Unaweza ukawa mzuri kwenye taaluma tofauti lakini kwenye mapenzi wewe ni wa hovyo. Mapenzi yanawasumbua wale. Wanafaa kuacha huu upuuzi, wote. Huu upuuzi unawachafua wote hadi wanaonekana waliokata tamaa. Hawapaswi kuongea vile vitu walivyoviongea,” Mwijaku alisema.

View Comments