In Summary

• Shabiki huyo pia alisema kwamba kitu kizuri katika ndoa za mitala ni kwamba watoto huwa wanapendana licha ya kwamba kina mama huchukiana.

• Nyamu alimjibu akisema kwamba yeye kumtaja katika sentensi moja na chuki dhidi ya mwanamke mwenzake kisa mapenzi wala hawezi patikana.

Karen Nyamu asisitiza hana chuki dhidi ya Nderitu Edday.
Image: Instagram

Seneta Karen Nyamu amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba hawezi kuwa na chuki dhidi ya mke mwenza Edday Nderitu.

Nyamu alisema haya wakati alikuwa anamjibu shabiki mmoja ambaye alitoa maoni yake kwenye chapisho lake mitandaoni.

Karen Nyamu alikuwa amepakia video akiwa na mtoto wake wa kiume kwenye TikTok wakati shabiki mmoja alitoa maoni akisema kwamba mvulana huyo atakuwa rafiki mkubwa kwa ndugu zake kutoka mama mwingine – Edday Nderitu.

Shabiki huyo pia alisema kwamba kitu kizuri katika ndoa za mitala ni kwamba watoto huwa wanapendana licha ya kwamba kina mama huchukiana.

Nyamu alimjibu akisema kwamba yeye kumtaja katika sentensi moja na chuki dhidi ya mwanamke mwenzake kisa mapenzi wala hawezi patikana.

“Huyu atakuwa na ukaribu mkali na ndugu zake wakubwa, uzuri wamama huchukiana lakini watoto,watoto watapendana hata iweje,” Faith Kamundi aliandika.

“Mimi usini hesabu hapo kwa chuki pls,” Karen Nyamu alimjibu.

Hii si mara ya kwanza kwa seneta huyo maalum kuweka wazi kwamba hana chuki dhidi ya mke mwenza licha ya wawili hao kuonekana hadharani wakitofautiana kisa mapenzi ya baba watoto wao Samidoh.

Nyamu na Nderitu kwa wakati mmoja walifikia pabaya nusra kuparurana hadharani mjini Dubai wakati Samidoh alikuwa na shoo mwishoni mwa mwaka jana.

Tofauti zao zilikwenda mbali Zaidi kumpelekea mke wa kwanza kubwaga manyanga na kwenda Marekani akiongozana na wanawe watatu huku akisema kwamba aliamua kuchukua uamuzi huo ili kumuacha Samidoh mikononi mwa mwanamke ambaye alikuwa na haja kubwa kukaa naye – Karen Nyamu.

Nderitu aliweka wazi tena kwa kusisitiza kwamba hawezi kubali kuwalea wanawe katika ndoa yeney mke Zaidi ya mmoja, licha ya kwamba mumewe anaonekana kuganda kwa penzi la Karen Nyamu ambaye ni kama mke wa pili na tayari wan watoto wawili pamoja.

 

View Comments