In Summary

• Stevo alikiri ni kweli Vishy ni mzuri na anajua kuvaa kisasa mitandaoni ikilingansihwa na mwenzake Ngesh wa Vasha lakini yeye akasisitiza kwamba hataki mtu wa mapambo.

Stevo na Pritty
Image: Instagram

Msanii Stevo Simple Boy kwa mara ya kwanza amejibu kauli ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Pritty Vishy baada ya kusema kwamba wakipendana na msanii chipukizi wa Kaveve Kazoze, Ngesh wa Vasha, watazaa watoto ‘tuveve tusimple’.

 Katika mazungumzo na waandishi wa habari za mitandaoni wakati alikuwa anautambulisha wimbo wake mpya alioshirikishwa na msanii wa injili David Wonder, Stevo Simple Boy alisema kwamba Vishy ni mzuri lakini si yule wa kuweza kuwekwa ndani kama mke.

Msanii huyo wa ‘Mihadarati’ alimlinganisha Vishy na Ngesh wa Vasha akisema kwamba mmoja anatajwa kuwa mbaya lakini ndiye anaweza kuwa mke huku mwingine akiwa mzuri lakini asiyeweza kufugika, akitumia nadharia ya punda na pundamilia.

Japo hakumtaja mtu, alisema kuwa yeye hawezi kuyumbishwa na maneno ya watu kusema kwamba kuendea Kaveve Kazoze ni kama kujishusha hadhi kutoka pale ambapo Vishy alimfikisha.

“Unafaa watu wanafaa kuelewa kuna pundamilia na punda. Mimi sitaji mtu lakini pundamilia ni kivutio cha watalii lakini punda huwa siku zote anadharauliwa lakini huwa ni msaidizi wa watu pale nyumbani. Kati ya punda na pundamilia nachagua punda.” Stevo alisema.

Stevo alikiri ni kweli Vishy ni mzuri na anajua kuvaa kisasa mitandaoni ikilingansihwa na mwenzake Ngesh wa Vasha lakini yeye akasisitiza kwamba hataki mtu wa mapambo tu bali anataka mtu wa kuweza kufugika nyumbani.

Siku mbili zilizopita, Pritty Vishy alikejeli uhusiano wa Kaveve Kazoze na Stevo Simple Boy akisema kuwa wawili hao ikiwa kweli wataishia kwenye ndoa watoto watakuwa tuveve tusimple.

“Watoto wa Kaveve Kazoze­­+Stevo Simple Boy=Tuveve Tusimple” aliandika kwenye Instastory yake.

View Comments