In Summary

• Harmonize alisema kwamba wakati wanaketi chini kuchora mpango mzima, alinunua vifaa vingi.

• Msanii huyo hata hivyo alisema kuwa hiyo haina maana kwamba ako na hisa katika kampuni ya Wasafi.

Harmonize aibua mapya kuhusu kuanzishwa kwa Wasafi.
Image: Instagram

Msanii Harmonize akimefichua kwamba kuanzishwa kwa vituo vya redio na runinga ya Wasafi lilikuwa ni wazo lake enzi zile wakiwa na Diamond katika kampuni ya Wasafi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makazi yake ya Konde Village wakati wa tafrija ya ngoma yake ya Singo Again Remix aliyomshirikisha Ruger kutoka Nigeria, msanii huyo alifichua kwamba hilo lilikuwa ni wazo lake.

Harmonize alisema kwamba wakati wanaketi chini kuchora mpango mzima, alinunua vifaa vingi lakini baadae alipotoka aliviacha vyote na wala hakubeba haka kifaa kimoja.

“Wazo la kwanza lilikuwa ni chaneli ya mitandaoni na hilo lilikuwa wazo letu pamoja. Kufikia muda mimi nilisafiri kwenda Italia nilikuwa nimenunua vifaa ikiwemo na mashine za DJ na mashine nyingine nyingi, na tulipoanza tukasema kwa nini tusitafute mtu tukafanya naye kwa pamoja.. singependa kumtaja mtu huyo.. lakini vifaa vilikuwepo kwa sababu nilikuwa nimenunua mimi,” alisema.

“Kwa hiyo tukapata mtu wa kushirikiana naye, vifaa vilikuwepo na mimi sikuvihitaji tena kwa sababu sikuwa na mpango wa kufanya redio. Sikuvuiza, niliacha kila kitu pale nilipoondoka niliondoka mwenyewe kama mimi,” aliongeza.

Msanii huyo hata hivyo alisema kuwa hiyo haina maana kwamba ako na hisa katika kampuni ya Wasafi akisema aliondoka mwenyewe kwa sababu alichokuwa anakitaka si kingine Zaidi ya Amani tu.

“Mimi nimeondoka mimi kwa sababu nilichokihitaji ni Amani na sitaki kuibua kitu chochote kwa sababu hainisadii chochote. Ni hadithi ya muda mrefu. Kuzungumzia redio ilikuwa ni wazo langu na nilishafika hadi kununua vifaa lakini nikaisitiza kwa sababu niliona kuna vitu vingi ambavyo watu wa Mtwara wanahitaji,” alisema.

View Comments