In Summary

• “Sinywi tena pombe kuanzia kesho, BFF tunza siri zangu nimeongea sana,” Harmonize aliandika.

Harmonize.
Image: Instagram

Siku mbili baada ya Harmonize kuchombeza urafiki na aliyekuwa mpenzi wa Haji Manara, Harmonize safari hii amefuma mkuki katika moyo wa Diamond baada ya kumtambulisha aliyekuwa mpenzi wake, Hamisa Mobetto kama rafiki wake wa karibu – BFF.

Harmonize alianza kwa kupakia picha ya Hamisa Mobetto ambayo inamuonesha akiwa ameketi kwenye ndege, kwenye viwiko amepakata mto na viganjani ameshikilia simu kwa tabasamu akiwa kama anatumiana ujumbe na mtu.

“Kutana na BFF wangu mpya,” Harmonize aliandika.

Hamisa naye si mchache. Aliichukua picha hiyo kutoka kwa Instastory ya Harmonize na kuirepost akiandika “BFF” na kuifuatisha na emoji za makopa ya mapenzi.

Na kama sumu hiyo haijatosha kwa Diamond, Harmonize na Mobetto walikutana kwenye baa ya starehe na Harmonize aliweka video wakiwa katika mkao wa kimahaba na mrembo huyo mama wa watoto wawili na kuanduika;

“BFF alipata video yangu wakati niko kwenye mambo yangu. Ndio maana naacha pombe.”

Wawili hao katika video nyingine tena walionekana wakigonga cheers za vinywaji kwenye glasi na kama njia moja ya kuhitimisha uzinduzi wa goma ambalo amelitajak uwa kubwa kabisa katika mwaka 2023, na kusema kwamba hiyo ndio mara ya mwisho anakunywa pombe, kwa sababu tu ya BFF wake mpya.

“Sinywi tena pombe kuanzia kesho, BFF tunza siri zangu nimeongea sana,” Harmonize aliandika huku Mobetto naye akipakia video hiyo wakiwa pamoja na kutetea mkao huo akisema, “Namzuia BFF asilewe jamani.”

Wawili hao walionekana katika siha nzuri kabisa ya kulipiga tafrija ikiwa ni siku mbili baada ya Harmonize kumpokea kutoka uwanja wa ndege Rushaynah – aliyekuwa mke wa Haji Manara.

Harmonize na Rushaynah walikuwa na muda wa kukumbukwa kwenye hari lake akimuendesha kuelekea nyumbani kwake ambapo alikuwa na pool party kwa ajili ya ngoma yake ya Single Again Remix aliyomshirikisha Ruger kutoka Nigeria.

View Comments