In Summary

• Kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, aliteuliwa katika vitengo zaidi ya vitatu huku Zuchu akiteuliwa katika kitengo cha mcheza densi.

Janet Otieno na Nadia Mukami
Image: Instagram

Wakali wa muziki duniani Trace wamewataja walioteuliwa kuwania tuzo za kwanza kabisa za Trace Awards barani Afrika, tukio la moja kwa moja na tamasha la kimataifa la televisheni linaloadhimisha ubunifu, vipaji na ushawishi wa muziki na wasanii wa Kiafrika na Afro.

Inafanyika moja kwa moja tarehe 21 Oktoba 2023 katika BK Arena, Kigali, Rwanda.

 “Kuanzia Kaskazini hadi Kusini, kutoka Mashariki hadi Magharibi, bara zima la Afrika litawakilishwa na wasanii wake bora katika Tuzo za Trace, kuonyesha ubora na utofauti wa muziki wa Afro-centric katika aina kama vile Afrobeat, Dancehall, Hip Hop, Afro-pop, Mbalax, Amapiano, Zouk, Kizomba, Genge, Coupé Décalé, Bongo Flava, Soukous, Gospel, Rap, Rai, Kompa, R&B, na Rumba,” Ilisema taarifa kwenye tovuti ya Trace TV.

Wanaoshindana katika vipengele 22 vya tuzo ni wasanii wanaouza zaidi kutoka zaidi ya nchi thelathini za Afrika, Amerika Kusini, Caribbean, Bahari ya Hindi na Ulaya zikiwemo Algeria, Angola, Brazil, Cameroon, Cape Verde, Comoro, DRC, Ufaransa, French Guiana, Gabon, Ghana, Guadeloupe, Haiti, Ivory Coast, Jamaica, Kenya, Madagascar, Martinique, Mayotte, Mauritius, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Reunion, Rwanda, Senegal, Afrika Kusini, Swaziland, Tanzania, Tunisia, Uingereza na Uganda. Washindi watajinyakulia Tuzo moja au zaidi za Trace Awards - vipande vya kipekee vya sanaa vilivyobuniwa na mchongaji na mbunifu maarufu wa Kongo, Dora Prevost, ilisema Zaidi taarifa hiyo.

Katika orodha hiyo ndefu, taifa la Kenya litawakilishwa na wasanii wawili pekee wa kike – Nadia Mukami na mkongwe wa miziki ya injili Janet Otieno.

Mukami ameteuliwa kuwania tuzo ya msanii bora wa kike Afrika na atamenyana na wakali kama Soraia Ramos wa Cape Verde, Josey kutoka Ivory Coast, Viviane Chidid wa Senegal na tishio mara mbili la Tiwa Savage na Arya Starr (Nigeria).

Kwa upande wake, Janet Otieno atamenyana na wainjilisti wenzake katika kitengo cha msanii bora wa injili, wakiwemo Benjamin Dube wa Afrika Kusini, Levixone wa Uganda, KS Bloom kutoka Ivory Coast na Moses Bliss kutoka Nigeria.

Hii hapa orodha kamilifu ya vitengo mbalimbali;

Msanii bora wa kiume Asake (Nigeria) 

Burna Boy (Nigeria)

Davido (Nigeria)

Diamond Platnumz (Tanzania)

Didi B (Ivory Coast)

K.O (South Africa)

Rema (Nigeria)

Msanii bora wa kike

Ayra Starr (Nigeria)

Josey (Ivory Coast)

Nadia Mukami (Kenya)

Soraia Ramos (Cape Verde)

Tiwa Savage (Nigeria)

Viviane Chidid (Senegal)

 Wimbo wa mwaka

“BKBN” – Soraia Ramos (Cape Verde)

“People” – Libianca (Cameroon)

“Suavemente” – Soolking (France)

“Encre” – Emma’a (Gabon)

“Sugarcane” – Camidoh (Ghana)

“Last Last” – Burna Boy (Nigeria)

“Rush” – Ayra Starr (Nigeria)

“Calm Down” – Rema (Nigeria)

“Peru” – Fireboy DML (Nigeria) na Ed Sheeran (UK)

“Sete” – K.O (South Africa)

“Cough” – Kizz Daniel (Nigeria)

“MORTEL 06” – Innoss’B (Ivory Coast)

 

Video bora ya mwaka

“2 Sugar” – Wizkid (Nigeria) feat. Ayra Starr (Nigeria)

“Baddie” – Yemi Alade (Nigeria)

“Kpaflotage” – Suspect 95 (Ivory Coast)

“Loaded” – Tiwa Savage(Nigeria) & Asake (Nigeria)

“Ronda” – Blxckie (South Africa)

“Tombolo” – Kalash (Martinique) 

"Yatapita” – Diamond Platnumz (Tanzania)

 

Msanii chipukizi bora

Azawi (Uganda)

Krys M (Cameroon)

Libianca (Cameroon)

Nissi (Nigeria)

Odumodublvck (Nigeria)

Pabi Cooper (South Africa)

Roselyne Layo (Ivory Coast)

Kolabo bora

“Many Ways” – BNXN (Nigeria) with Wizkid (Nigeria)

“Mine” – Show Dem Camp (Nigeria) with Oxlade (Nigeria)

“Peru” – Fireboy DML (Nigeria) with Ed Sheeran (UK)

“Second Sermon” – Black Sherif (Ghana) with Burna Boy (Nigeria)

“Sete” – K.O (South Africa) na Young Stunna (South Africa), Blxckie (South Africa)

“Stamina” – Tiwa Savage with Ayra Starr (Nigeria) & Young Jonn (Nigeria)

“Trumpet” – Olamide (Nigeria) with Ckay (Nigeria)

“Unavailable” – Davido (Nigeria) with Musa Keys (South Africa)

 

DJ Bora

Danni Gato (Cape Verde)

DJ BDK (Ivory Coast)

DJ Illans (France)

DJ Spinall (Nigeria)

Michael Brun (Haiti)

Uncle Waffles (Swaziland)

PRODUSA BORA

DJ Maphorisa (South Africa)

Juls (Ghana)

Kabza de Small (South Africa)

Kel-P (Nigeria)

Tamsir (Ivory Coast)

 

Msanii bora wa injili

Benjamin Dube (South Africa)

Janet Otieno (Kenya) 

KS Bloom (Ivory Coast)

Levixone (Uganda)

Moses Bliss (Nigeria)

 

Msanii bora wa kutumbuiza moja kwa moja

Burna Boy (Nigeria)

Fally Ipupa (DRC)

Musa Keys (South Africa)

The Compozers (Nigeria)

Wizkid (Nigeria)

Yemi Alade (Nigeria)

Mcheza densi bora

Robot Boii (South Africa)

Tayc (France)

Uganda Ghetto Kids (Uganda)

Yemi Alade (Nigeria)

Zuchu (Tanzania)

 

Msanii bora wa Kiafrika - Anglophone

Asake (Nigeria)

Ayra Starr (Nigeria)

Black Sherif (Ghana)

Davido (Nigeria)

Diamond Platnumz (Tanzania)

Fireboy DML (Nigeria)

 

Msanii bora wa Kiafrika - Francophone

Didi B (Ivory Coast)

Emma’a (Gabon)

Fally Ipupa (DRC)

KO-C (Cameroon)

Locko (Cameroon)

Serge Beynaud (Ivory Coast)

Viviane Chidid (Senegal)

 

Msanii bora wa Kiafrika - Lusophone

Gerilson Insrael (Angola)

Lisandro Cuxi (Cape Verde)

Perola (Angola)

Plutonio (Mozambique)

Soraia Ramos (Cape Verde)

Albamu bora ya mwaka

“DNK”- Aya Nakamura (France)

“Love Damini” – Burna Boy (Nigeria)

“Maverick” – Kizz Daniel (Nigeria)

“More Love, Less Ego” – Wizkid (Nigeria)

“Timeless” – Davido (Nigeria)

“Work of Art” – Asake (Nigeria)

 

 

View Comments