In Summary

• “Wakenya msinitag kwa vita vyenu na watanzania, wamepokea na wanazipenda nyimbo zangu, wengine wa wasanii kutoka Tz ni marafiki Zangu," - Akothee.

Akothee.
Image: Instagram

Katika muda wa wiki moja iliyopita, wasanii wa Tanzania na wale wa Kenya wakiwemo pia mashabiki wamekuwa wakishambuliana mitandaoni katika mzozo ambao uliwashwa moto na rapa Khaligraph Jones.

Wiki jana, Jones alifanya ngoma ya kutupa vijembe kwa Sanaa ya HipHop ya Tanzania akisema kwamba Sanaa hiyo imefariki muda mrefu na hata kutoa makataa ya saa 24 kwa wasanii wa Bongo HipHip kumjibu kama wako tayari kumenyana kwa maneno ya kufoka kimuziki na yeye.

Kauli hiyo iliwachemua wasanii wengi wa Tanzania ambao wengi wameonekana kujisatiti kwa kuachia diss track za kuchekesha kumjibu Khaligraph Jones.

Lakini pia mzozo huu wa maneno umekumbatiwa na mashabiki baina ya mataifa haya mawili pamoja pia na wasanii wengine wakiwemo Stevo Simple Boy, Breeder LW miongoni mwa wengine ambao wameonekana kumuunga mkono Khaligraph kwamba hakuna rapa wa Tanzania anayeweza kumng’oa kileleni.

Ikiwa ilitarajiwa kuwa wasanii wengi wa Kenya wangemuunga mkono Khaligraph, kwa msanii Akothee hali ni tofauti.

Akothee kupitia Instagram ameweka wazi kwamba hawezi kujiingiza kwenye mzozo huo wa vita vya maneno baina ya mataifa hayo mawili, pia akitolea sababu za kuchagua hivyo.

Akothee alisema kwamba hataki kabisa mtu yeyote kumtegi katika vita hiyo ya maneno kwa sababu yeye ana mashabiki wengi kutoka Tanzania ambao wanampenda lakini pia akasema Watanzania ni majirani zake wema tu.

Wakenya msinitag kwa vita vyenu na watanzania, wamepokea na wanazipenda nyimbo zangu, wengine wa wasanii kutoka Tz ni marafiki Zangu, mkitukanwa na watanzania mini siko na Nyinyi,😂😂😂😂😂 Tena ni majirani Zangu huko Migori na Mombasa pia 😂😂 Shauri Zenu,” Akothee alijiondoa kwenye sakata hilo.

Alisema kwamba mashabiki wengi wa Kenya walishamuondoa kwenye ramani ya wasanii wakisema kwamba yeye si msanii bali ni mwanasarakasi, na hivyo akajizolea mashabiki wengi kutoka Tanzania ambao sasa Wakenya wanataka ajiunga na Khaligraph katika kuwatupia vijembe.

“Kwanza mlishasema mimi siimbi. Mimi Watanzania ni marafiki zangu kwa hiyo msiniwekelee,” aliongeza.

View Comments