In Summary

• Harmonize aliandika haya kupitia Instagram bila kumtaja jina Diamond moja kwa moja lakini kwa ishara zote hili dongo lilikuwa limeelekezwa moja kwa moja kwake Diamond.

Harmonize na Diamond
Image: Insta

Harmonize hachoki kumchokoza Diamond, tangu mwishoni mwa mwaka 2019 wawili hao walipotofautiana kimuziki kumpeleka Harmonize kuondoka kishari na kuanzisha lebo yake ya Konde.

Safari hii msanii huyo ametopa dongo tena kwenye kambi ya WCB Wasafi akisema kwamba Diamond licha ya uwepo wake kwenye Sanaa ya muziki kwa Zaidi ya miaka kumi, lakini bado hawezi kuwafikia wasanii wa Nigeria ambao wana miaka miwili tu kwenye muziki.

Harmonize aliandika haya kupitia Instagram bila kumtaja jina Diamond moja kwa moja lakini kwa ishara zote hili dongo lilikuwa limeelekezwa moja kwa moja kwake Diamond.

Harmonize aliwahimiza wasanii wa Afrika Mashariki kujikita katika kuachia miziki iliyotungwa kwa lugha ya Kiingereza akisema kuwa hiyo ndio njia pekee ya kuwajumuisha na kuwavutia mashabiki wao kutoka mataifa ya ughaibuni ambao hawaelewi Kiswahili.

Kaitka usanjari huo, Harmonize pia alimshambulia Diamond kichini chini akisema kwamba baada ya kuazna kuonesha ufanisi katika muziki wake kimataifa, sasa hawezi kupewa shoo ya kutumbuiza mchana ili wasanii wakubwa wakisubiri kutumbuiza usiku.

 Itakumbukwa juzi kule Detroit Marekani, Diamond alionekana akitumbuiza majira ya mchana wakati wasanii tajika waliweka pembeni ili kutumbuiza nyakati za usiku wakati umati umeshona kwenye ukumbi.

“Najivunia sana kwa wasanii wa Afrika Mashariki, sasa kuna wasanii wanaweza imba Kiswahili, wengine Kiiingereza na wengine kutuia lugha zote. Watu wabayaaaaa, Afrika Mashariki tunakuja, na hii ndio njia pekee ya kuhakikisha kwamba hatutakuwa tunapewa shoo za adhuhuri na alasiri katika matamasha makubwa…. Hatutafungua shoo tena ndugu zangu wa Afrika Mashariki… sasa msanii wa Nigeria mwenye miaka miwili tu kwenye muziki ni mkubwa kuliko msanii wa Afrika Mashariki ambaye amekaa kwenye gemu kwa Zaidi ya miaka 10,” Harmonize alimfuma Diamond kifuani.

Msanii huyo amekuwa akijipiga kifua kutokana na ufanisi mkubwa ambao wimbo wake wa Single Again umejizolea katika miezi mitano tangu kutoka.

Wimbo huo ambao ameimba kwa lugha ya Kiingereza umekuwa hit kubwa sana katika mataifa mengi tu mpaka kumvutia msanii Ruger kutoka Nigeria kumshirikisha katika remix ambayo pia inazidi kupaa kwa kasi ya kupendeza kwenye majukwaa ya kidijitali ya kupakua miziki.

View Comments