In Summary

• “Mpendwa Arteta, hii ndio safu tunayotarajia Jumapili dhidi ya Manchester United, hiyo ndiyo tu tunayouliza,” Gidi aliandika.

Gidi na Arteta.
Image: Maktaba

Mtamtangazaji wa Radio Jambo Gidi Ogidi amemuandikia barua ya dhati kocha wa timu anayoishabikia ya Arsenal, Mikel Arteta kuhusu kikosi ambapo yeye kama shabiki angepedna kichezeshwe dhidi ya Manchester United katika mecho yao ya Jumapili wikendi hii.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Gidi alituma ujumbe huo kwa Arteta akimtaka kuchagua kikosi cha wachezaji aliowataja akisema kwamba ujumbe huo ni kwa niaba ya mashabiki wote wa Arsenal ambao hawajafurahishwa na viwango vya mchezo wa Arsenal tangu msimu kuanza wiki tatu zilizopita.

“Mpendwa Arteta, hii ndio safu tunayotarajia Jumapili dhidi ya Manchester United, hiyo ndiyo tu tunayouliza,” Gidi aliandika.

Katika kikosi ambacho alikiteuwa, Gidi alimfungia nje sajili mpya Kai Havertz aliyenunuliwa kutoka Chelsea na ambaye licha ya kukabidhiwa muda mwingi uwanjani na Arteta, viwango vyake vya soka havijawaridhisha mashabiki wengi ambao wanahoji ni kwa nini Arteta anampa muda mwingi uwanjani hali ya kuwa haoneshi sababu ya kustahili muda huo.

Katika safu ya ushambuliaji, Gidi aliweka mshambulizi Gabriel Jusus ambaye mwishoni mwa wiki jana alitajwa kurejea katika mazoezi, akishirikiana na winga Matinelli na Saka.

Kwenye safu ya kati baada ya kumtupa nje Havertz, Gidi aliweka nahodha Odegaard, sajili mpya Declan Rice na kiungo kutoka Ghana Thomas Partey ambaye amekuwa akichezeshwa kwenye safu ya ukabaji ili kutoa nafasi kwa Havertz kwenye kiungo.

Mstari wa nyuma Gidi alimtaka Arteta kuwachezesha Zinchenko, Gabriel, Saliba na Ben White huku langoni akimpa nafasi Ramsdel.

Kama wewe ni shabiki wa Arsenal, unakubaliana na kikosi alichokitoa Gidi?

View Comments