In Summary

• Walisema kwamba wanapopiga kisengere nyuma hadi mwaka 2005 waliposema ‘ndio’ kwa kila mmoja, wanajawa na furaha.

• Mwisho kabisa wawili hao waliwashukuru mashabiki wao kwa kuwaminia na kuwachukulia kama mfano hai katika ndoa zao.

Nameless na Wahu.
Image: Instagram

The Mathenges, kama wanavyojiita wasanii Wahu na Nameless leo hii Septemba 10 kwa mara nyingine tena wanajawa na kumbukumbu nzuri kwani ndio siku walifunga harusi miaka 18 iliyopita.

Wanandoa hao wanaosherehekea Zaidi mitandaoni na kuchukuliwa kama kielelezo cha jamii katika suala la kusawazisha familia na umaarufu wamesherehekea kudumisha miaka 18 katika ndoa kwa ujumbe wa pamoja uliotiwa nakshi.

Katika ujumbe wa pamoja katika mitandao yao ya kijamii, walisema kwamba sasa wanaweza jivunia kwani ndoa yao imefikisha umri wa miaka 18 ambao nchini Kenya kisheria ni umri wa kuonesha kwamba mtu si mtoto tena bali amekomaa katika utu uzima.

Walisema kwamba wanapopiga kisengere nyuma hadi mwaka 2005 waliposema ‘ndio’ kwa kila mmoja, wanajawa na furaha.

“Leo tunasherehekea miaka 18 ya ndoa🙏🏿 , Ndoa yetu imekuwa Adult buana!! 😁😎Hatuwezi kujizuia kutafakari kwa Shukrani katika safari ya hali ya juu na hali ya chini, shangwe zisizokumbukwa na maumivu ya bahati mbaya ambayo tumeshiriki pamoja,” walisema.

Hata hivyo, hawakukosa kukiri kwamba katika miaka hiyo yote, hawajapitia changamoto.

Walisema kwamba wamekosana mara nyingi na hata kupigana vita vya maneno lakini hilo halikuweza kuyumbisha muunganiko wao.

“Tumepigana na kusuluhishana, tumekuwa na kukosa-Kuelewana lakini kila wakati tulijitahidi kuelewana kwa miaka mingi. Lakini ni nini hakika, sisi ni watu binafsi na washirika bora kwa sababu ya muungano huu,” walisema.

Mwisho kabisa wawili hao waliwashukuru mashabiki wao kwa kuwaminia na kuwachukulia kama mfano hai katika ndoa zao.

“Asante familia kwa kuonyesha upendo wa M'z katika safari yetu yote. Furaha kwa mtoto wa miaka 18.️ Hapa kuna milele zaidi!” walisema.

Mwaka jana wakisherehekea miaka 17 ya ndoa, Wahu alipakia video akionesha jinsi walikuwa na tafrija ya kitamaduni baada ya harusi.

Video hiyo ilionyesha Wahu akiwasili kwenye ukumbi wa harusi kwa mashua, akiwa amevalia nguo nyeupe na ngozi ya mnyama ya kahawia.

Msanii huyo alifichua kwamba kabla ya kufunga ndoa ya Nameless mwaka 2005, walikuwa wamechumbiana kwa miaka minane.

Kwa hiyo ni sahihi kusema kwamba mahusiano ya wawili hao wenye umaarufu mkubwa yamedumu kwa miaka 26.

 

View Comments