In Summary

• Akitetea msimamo wake, Omondi alisema kuwa mswada wa kifedha uliopitishwa kuwa sheria bungeni unaathiri vijana kote nchini.

Eric Omondi na Jalang'o
Image: Screenshot

Mchekeshaji ambaye pia ni mwanaharakati Eric Omondi amesema wazi wazi kwamba Jalang’o – rafiki yake wa muda mrefu – hafanyii kazi wananchi wa Lang’ata waliomchagulia kwenda bungeni.

Akizungumza na Obinaa katika mahojiano kwenye chaneli yake, Omondi alisema kwamba Kenya wabunge wanaofanya kazi haswa katika maenebunge yaliyoko katika kaunti ya Nairobi ni wawili tu – Babu Owino wa Embakasi Mashariki na Ronald Kauari wa Kasarani.

Akieleza kwa nini haoni kama Jalang’o anafanya kazi Lang’ata, Omondi alisema kuwa mbunge yeyote ambaye alipiga kura ya kuunga mkono mswada wa fedha wa mwaka 2023 ili wanablogu kutozwa ushuru Zaidi huyo hafanyi kazi hata kidogo.

“Hakuna mbunge hata mmoja anayefanya kazi ukiachia mbali Babu Owino, na huyu wa Kasarani namfuata Instagram naona jinsi anavyofanya kazi. Siamini kama Jalas anafanay kazi kwa sababu mtu yeyote aliyepigia kura mswada wa fedha, mbunge yeyote aliyepiga kura kutozwa ushuru kwa wakuza maudhui…” alisema.

Akitetea msimamo wake, Omondi alisema kuwa mswada wa kifedha uliopitishwa kuwa sheria bungeni unaathiri vijana kote nchini.

“Chochote ambacho unakifanya katika eneo bunge huathiri vijana wadogo katika eneo hilo. Na mswada ule ni kitu ambacho kitakuja kuwaathiri watoto wa watoto wetu. Kwa hiyo huo nsio ulikuwa muda wao wa kusema hapana,” Omondi alieleza.

Hata hivyo, mchekeshaji huyo alikanusha kwamba uanaharakati ambao anaufanya analenga kuutumia kujipigia debe kwa ajili ya uchaguzi wa 2027.

Alipoulizwa kama atasimama kumenyana na Jalang’o Lang’ata, Omondi alikwepa kujibu swali hilo moja kwa moja akisisitiza kwamba anachokiamini ni kwamba sauti ya watu ni sauti ya Mungu lakini akasema hajawahi hata siku moja kuzungumzia mambo ya Lang’ata.

Alisema kwamba anaamini popote atakaposimama kuwania wadhifa wowote ule, kiongozi ambaye atakuwa anakalia kiti hicho moja kwa moja anaenda nyumbani mapema.

View Comments