In Summary

• Mwanamume huyo alikuwa anahadithia hili katika video moja ambayo imepakiwa na blogu ya udaku nchini humo ambapo mchungaji alimtaka kusimulia jinsi walivyokutana.

Wakfu wajitolea kufadhili mahari kwa ajili ya ndoa
Image: maktaba

Mwanamume mmoja nchini Tanzania alitokwa na machozi ya furaha baada ya kutimiza ndoto yake ya muda mrefu kwa kufunga ndoa ya kanisani na mwanamke ambaye alimtumia ujumbe kwenye DMs zake mitandaoni kwa kipindi cha mwaka mzima bila kujibiwa.

Mwanamume huyo alikuwa anahadithia hili katika video moja ambayo imepakiwa na blogu ya udaku nchini humo ambapo mchungaji alimtaka kusimulia jinsi walivyokutana.

“Kwanza ilikuwa ni Mwanza ambapo ndipo nilipomuona. Ilikuwa ni dukani na kusema kweli nilikuwa naita sikuwa na nia ya kuingia kweney hilo duka. Nilikuwa naenda kwenye duka lingine ambalo wamepakana kununua bidhaa Fulani. Alikuwa kwenye duka la rafiki yake,” mwanaume huyo mwenye furaha alieleza.

“Nilipofika dukani nikawa nimemuona lakini sikumsemesha na baadae sikujua kama nitaweza kuonana naye tena maana na mimi sio kwamba nitakuwepo kwenye lile duka mara kwa mara,” aliongeza.

Alisema baadae aliona rafiki ya huyo mrembo mwenye duka lile akiwa amemtegi kwenye chapisho la Instagram na hapo ndipo alipata nafasi nzuri ya kumtumia ujumbe wa faragha kwenye DM.

“Nilivyomuona kwenye ukurasa wa rafiki yake wa Instagram nikakumbuka huyo hapa nilimuona siku ile. Basi nikamtext lakini hakujibu. Ilinichukua karibia mwaka mzima kujibiwa kwa sababu ilikuwa ni 2019…” alieleza.

 

View Comments