In Summary

โ€ข Kabla ya kuoana rasmi mwaka 2005, walidokeza kwamba walikuwa wamechumbiana kwa miaka 8.

Nameless na Wahu
Image: Facebook

Familia ya maceleb, Nameless na Wahu wiki hii wanasherehekea miaka 18 tangu walipofunga harusi mwaka 2005.

Wasanii hao wawili ambao wanatajwa kuwa kielelezo bora kwa jamii si tu katika muziki bali pia katika masiha yao ya ndoa na familia kwa jumla sasa wamedokeza kwamba hivi karibuni watakuwa wanashiriki hadithi 18 za kupotosha kuhusu ndoa ambazo wamejifunza katika safari yao ya miaka 18 kuwa si za kweli.

Nameless kupitia kurasa zake mitandaoni alianza kwa kuwashukuru wafuasi na mashabiki wao waliowaandikia jumbe za kheri njema tangu wikendi na kusema kwamba wamezisoma zote japo hawawezi kuzijibu zote kwa sababu ya muda.

Aliweka wazi kwamba watakuwa wanashiriki hadithi hizo za kupotosha kuhusu ndoa kama njia moja ya kuwatia moyo mashabiki wao walioko katika ndoa na wale ambao wanafikiria kuingia katika ndoa.

โ€œFam, wazito, wadau,๐Ÿ˜Š asante kwa jumbe zote za moyo za pongezi kwa Maadhimisho haya ya Miaka 18 ya ndoa yetu! ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟโ™ฅ๏ธtumezisoma, ๐Ÿ™๐Ÿฟ TunawaAppretiate ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ... Halafu, Tunafikiria kushirikisha hadithi 18 za ndoa ambazo tumegundua kupitia miaka 18 ya ndoa kuwa sio za kweli. โ™‚๏ธ๐Ÿคฆ๐Ÿพโ€โ™‚๏ธsaidia wengine ๐Ÿ˜โ€ Nameless aliandika.

Kwa upande wa mkewe Wahu, alipakia kipande cha video Jumatatu na kuwataarifu mashabiki wao kwamba walikuwa wamefunga safari kwenda sehemu ambayo hata hivyo hawakutaja wakisema kuwa wanaenda kusherehekea miaka 18 katika ndoa.

View Comments