In Summary

• Samidoh alikwenda Australia kwa ajili ya shoo ya wikendi na baadae mpenzi huyo wake alimfuata kimya kimya.

• Katka moja ya video, walionekana wakiwa ndani ya teksi wakizuru kutoka sehemu moja kuelekea nyingine huku wakitabasamu kwa furaha.

samidoh na familia zake
Image: Insta

Wikendi iliyopita, tuliripiti kuhusu video iliyovujishwa kutoka nchini Australia ikimuonesha seneta maalum Karen Nyamu akicheza densi jukwaani na baba watoto wake Samidoh katika moja ya tamasha alilokuwa akitumbuiza.

Sasa Nyamu mwenyewe amethibitisha kuwa ni kweli yuko na Samidoh wake Australia baada ya kuapkia msururu wa video fupi kwenye Instagram Story yake wakiwa wanajivinjari kwenye ziara hiyo.

Samidoh alikwenda Australia kwa ajili ya shoo ya wikendi na baadae mpenzi huyo wake alimfuata kimya kimya.

Katka moja ya video, walionekana wakiwa ndani ya teksi wakizuru kutoka sehemu moja kuelekea nyingine huku wakitabasamu kwa furaha.

Nyamu alimuonesha Samidoh ambaye alikuwa ametulia kwenye kiti chake ndani ya teksi uso wake ukiwa umetajaa Amani ya nafsi.

Katika moja ya video, wawili hao walionesha mikono yao kila mmoja ameshika bilauri yenye sharubati na kugonga cheers kwa furaha kabla ya kupiga tama.

Wakati wapenzi hao wanajivinjari Australia, mke wa Samidoh ambaye aliondoka kwenda Marekani kwa kile alisema ‘nimemuacha Samidoh kwa mwanamke aliyehitaji kuwa naye’ aliwakosha mashabiki wake kwa kuonesha picha ya pamoja na wanawe wakiwa wanaota jua la alasiri.

Kuna vile jua ya hapa inachoma differently,” Edday Nderitu aliandika.

Mama huyo wa watoto watatu aliondoka miezi kadhaa iliyopita pamoja na wanawe baada ya kusindwa kustahimili vishindo vilivyokuwa vikifuma upande wake kutokana na mgogoro wa kimapenzi kati yake, mumewe Samidoh na Karen Nyamu ambaye pia ni mzazi mwenza na Samidoh.

 

View Comments