In Summary

•Pia alitumia fursa hiyo kuomba kukutanishwa na fundi ambaye anaweza kukarabati na kutengeneza upya jumba hilo lake la kifahari.

Akothee kuhusu kujenga jumba la kifahari kijijini
Image: insta

Msanii na mjasiriamali Akothee amekuwa mtu wa hivi punde kujitosa mazima katika gumzo ambalo limekuwa likiwakutanisha Wakenya mitandaoni kuhusu kujenga nyumba nzuri kijijini.

Gumzo hilo ambalo limekuwa likiendelea kwa Zaidi ya wiki mbili limevutia pande mbili, watu wakisema kuwa kujenga nyumba nyumbani kwenu kijijini hali ya kuwa asilimia kubwa ya maisha yako unaishi mjini ni sawa na kuwekeza katika mradi uliokufa.

Wengine wanaunga mkono kujenga kijijini wakisema kuwa huko ndiko mtu utarudi mwisho wa siku wakati maisha ya mjini ambayo aghalabu hayatabiriki yatakapokupiga dafrau.

Akothee anaonekana kuunga mkono kundi la pili na alifanya hivi kwa kuwaonesha mashabiki wake boma lake lenye maua safi na jumba la kifahari.

Kwa mujibu wa msanii huyo, watu wengi ambao wanang’aka mitandaoni kwamba kujenga kijijini ni kutupa pesa ndio wale ambao hawana makazi hata chumba kibovu kijijini mwao.

“Watu wasio na makazi kijijini ndio wanajiaminisha kuwa kuwa na jumba la kifahari kijijini ni ufujaji wa pesa na mtaji uliokufa. Ngoja nikuulize, akili yako na starehe iko wapi? Unaita wapi nyumbani? Jumba kubwa la kukodi katika mahali ambapo huwezi kuhusisha? Ghorofa katika mji wa kelele? Nini kinakufanya ufikiri kuwa nyumba ni mtaji uliokufa,” Akothee aliuliza mfululizo wa maswali.

Akothee ambaye ana mafanikio makubwa kutokana na muziki wake aliendelea mbele kwa kutoa maelezo Zaidi kuonesha madhara hasi ya kumiliki jumba mjini mbali na nyumbani kwenu.

“Ngoja nikuambie ubaya wa kuwa na jumba kubwa la kifahari iwe kijijini au mjini. Gharama ya matengenezo ni zaidi ya gharama ya kuijenga, ili nyumba yako ionekane hivi, lazima utumie pesa kuweka thamani ya uso,” Akothee alisema akirejelea jumba lake lililoonekana nadhifu.

Aliwataka wanaowapotosha watu dhidi ya kujenga kijijini kukoma na kuacha kila mtu kufanya maamuzi yake na mtaji wake mwenyewe.

Pia alitumia fursa hiyo kuomba kukutanishwa na fundi ambaye anaweza kukarabati na kutengeneza upya jumba hilo lake la kifahari.

“Tusidanganye, kama hauna nyumba kijijini Hauna period usikatishe tamaa watu wenye maono wanaotafuta akili timamu. Kwa sasa, nitambulishe kwa mbunifu mzuri wa mambo ya ndani, nahitaji kukarabati mtaji wangu ulio hai,” aliongeza.

View Comments