In Summary

• Owen amesema Willy Paul amekua mtu wa kujituma sana  tangia akichipukia.

• Alisema Willy ana kipawa cha kuimba na kusakata densi hali inayomweka juu ya wasanii wengine. 

Daddy Owen/Instagram

Msanii na mtunzi wa nyimbo za injili Daddy Owen Mwatia , amemusifia Willy  Paul kuwa  msanii maarufu nchini.

Amesema haya akihadithia safari ya kukua kwa Willy Paul kama msanii, alisema kwamba aliteseka sana kupata nafasi ya kuimba nyimbo zake wakati akianza taaluma ya muziki.

Owen amesema Willy Paul amekua mtu wa kujituma sana  tangia akiwa mchanga, kwa kuonyesha uwezo alio nao wa kuimba na kudensi kwa pamoja jambo ambalo anahisi linamshawishi kumtaja Willy Paul kama msanii bora.

"Sizungumzi kuhusu Willy Paul ambaye watu wengine huzungumzia, nazungumza kuhusu Willy Paul ambaye nimeshuhudia akikua, ambaye nikienda kutumbuiza nyimbo zangu,anapigania kuimba nyimbo zake kwenye shoo zangu."

Amemtaja kuwa msanii ambaye kufikia sasa anajua kuwa bora zaidi kulinganisha na wasanii wengine wa nchini.

"Mambo yote yakizingatiwa, kufikia leo nahisi kwamba Willy Paul ni mmoja wa wanamuziki mahiri nchini."

Hata hivyo Willy Paul ameupokea ujumbe wa Daddy Owen akisema kwamba sio wasanii wote wanaweza kusifia kazi ya msanii mwenza na kumshukuru  kwa sababu ya kuongea hisia zake kumhusu.

Katika ujumbe aliochapisha kwa ukurasa wake wa Instagram, alisema;

"@Daddyowen, hatuongei sana ila asante kwa kusema  haya kunihusu bwana! Umenitia moyo kwa njia kadhaa. Tunaishi katika ulimwengu ambao hakuna atakayekuambia kuwa unachokifanya ni kizuri. Barikiwa," 

Haya yanjiri siku chache baada ya Cassypool kuwakosoa wasanii wa nyimbo za injili akisema kwamba wameachilia tasnia ya nyimbo za injili kufifia nchini, kwa kile anachosema kutoshirikiana miongoni mwa wasanii hao.

 

View Comments