In Summary

• Scarlet katika ujumbe huo wa kutia wasiwasi kwa nchi alisema kwamba mtu anayepanga kutekeleza mauaji hayo kwa rais ni mwanasiasa.

Bola Tinubu na AKA
Image: Twitter

Mtumiaji wa X, @AhunnaScarlet, ambaye hapo awali aligonga vichwa vya habari baada ya screenshot za utabiri wake kuhusu kifo cha msanii wa Afrika Kusini, AKA mwaka 2021 amerudi tena na utabiri mpya.

Ahunna Scarlet safari hii amerudi na utabiri kwamba kuna njama ya kuuawa kwa rais wa Nigeria Bla Tinubu, ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu kuapishwa kuchukua mamlaka ya uongozi katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Ahunna alianza kuvuma sana mapema mwaka wa 2023 wakati unabii wake wa miaka miwili kuhusu jinsi mwimbaji wa Afrika Kusini AKA angekufa ulipotimia. Baadaye alitoa unabii mwingine kuhusu Tems ya Nigeria.

Katika ujumbe wake wa Twitter mnamo Alhamisi, Septemba 21, Ahunna alisema Mungu alimwambia Rais Tinubu ajihadhari na jaribio la mauaji kutoka kwa mwanasiasa kutoka Kusini-Kusini ambaye anatamani kuteuliwa.

Scarlet katika ujumbe huo wa kutia wasiwasi kwa nchi alisema kwamba mtu anayepanga kutekeleza mauaji hayo kwa rais ni mwanasiasa ambaye amenyimwa nafasi ya kuhudumu katika baraza la mawaziri.

“Mungu anasema: Rais wa Nigeria, Tinubu anapaswa kujihadhari na mauaji yatakayotekelezwa kwake kutoka kwa mwanasiasa kutoka Kusini Kusini ambaye anatamani sana kuteuliwa katika baraza lake la mawaziri. Kuna mpango wa kumuondoa baada ya uongozi wake wa kwanza; na hivyo; tumia tamaa kama mbadala wake,” Tweet hiyo ya Ahunna Scarlet ilisoma.

Itakumbukwa mrembo huyo ambaye anajitambulisha kama mtabiri na pia mchanganuzi wa masuala ya kisiasa aligonga vichwa vya habari Februari mwaka huu baada ya kifo cha msanii AKA.

Unabii uliotolewa tarehe 2 Mei 2021 sasa umeenea. Utabiri huo ulitolewa na mwanahabari wa kisiasa Ahunna Scarlet Ejiogu kwenye Twitter.

"Mungu anasema: Msanii wa Rap wa Afrika Kusini, AKA anapaswa kujihadhari na risasi ambayo itachukua maisha yake. Anapaswa kuepuka urafiki na mikusanyiko ya mafia la sivyo atakuwa shabaha #Afrika Kusini," ilisomeka tweet hiyo.

View Comments