In Summary

• Kila mtoto anahitaji Identity, nataka kuamini alikuwa na upuuzi wake unaendelea na kichwa chake - Akothee.

Akothee.
Image: Instagram

Msanii Akothee ambaye ni mama kwa watoto watano wenye baba tofauti amekuja na ushauri kwa kina mama ambao wanalea watoto bila kuwepo kwa kina baba kwa watoto hao.

Akothee katika ushauri wake, anahisi kina mama hao ambao wanaficha au kufungia watoto kuonana na kujuana na baba zao ni kujichimbia shimo la majanga katika siku za usoni katika maisha ya watoto hao.

Akothee alitoa maoni kwamba si vizuri kwa kina mama hao kuwafungia watoto kuonana na baba zao, haswa kama mtoto ni wa kike kwani huwezi jua kesho mtoto huyo anakua na akija kuwa mtu mzima vipi akikutana na babake – bila kujua kuwa ni baba – na kuchumbiana, pengine kuzaa mtoto pamoja.

“Nikimnyima nafasi ya kumuona mtoto wake, vipi ikiwa mtoto ni mwanamke na anaishia kuwa mpango wake wa kando au mke au babymama? Mama wanapaswa kuweka maumivu kando na kuangalia katika picha kubwa. Ulimwengu ni mdogo sana, usibebe maumivu yako ya pembetatu ya upendo kwenye maisha ya Watoto wako,” Msanii huyo alishauri.

Alisema kwamba ikiwa baba ametoroka mimba au ameamua kulea, si jukumu lake kuwafungia watoto kumjua baba yao kwani inafika kipindi katika maisha mtoto anataka utambulisho wa baba.

“Ndio nitafanya, kwa kuwa ujauzito unatuchukua sisi wawili., na kila mtoto anahitaji Identity, nataka kuamini alikuwa na upuuzi wake unaendelea na kichwa chake na amerudi kwenye akili zake 🙏Sina muda wa kujibu maswali. Siwezi kujibu na sina kumbukumbu sifuri kwa uwongo,” alisema.

Msanii huyo akiwashauri kina mama hao alisema kwamba kitu tu ambacho hawafai kumruhusu yule baba mtoto kufikia ni yeye mwenyewe kwani alishamuacha na maisha yakaendelea kivingine.

“Njia pekee ambayo sitampa ni mimi mwenyewe, kwa sababu ninaamini katika miaka 13 nimepona na kusonga mbele. Watoto watakugeuka na kwenda kuchukua hizo beats zilizokufa na itakuumiza zaidi.”

View Comments