In Summary

• Alienda mbele na kumtaka gavana Sakaja kuhakikisha kwamba wafanyibiashara hao wanapata sehemu mbadala ya kuendesha biashara.

Kanju walibomoa vibanda
Image: Insta

Mchekeshaji na mwanaharakati Eric Omondi amewasili katika eneo la Muthangari Drive kwenye barabara ya Waiyaki baada ya wafanyibiashara wadogo kudai kubomolewa vibanda vyao na watu waliotajwa kuwa ni maaskari wa kaunti ya Nairobi marufu kama Kanju.

Vibanda hivyo vilivyo mkabala ya makao makuu ya kampuni ya Safaricom vilibomolewa mapema wiki hii na wafanyibiashara wadogo Zaidi ya 20 ambao walikuwa wanatafuta riziki yao katika eneo hilo walibaki wakishika tama baada ya watu hao waliokuwa na fujo kuharibu mtaji wao.

Omondi alifika ili kuwafariji na kutoa maagizo matatu kwa gavana Sakaja akisema kwamba alipewa taarifa watu waliotekeleza ubomozi huo ni maaskari wa kaunti na hawakuwa wametoa notisi kwa wafanyibiashara hao.

“Nilipata wito wa dhiki kutoka kwa wafanyabiashara wa Soko la Muthangari kuhusu shambulio la watu waliokuja na Kuharibu Biashara zao Ndogo Jana. Hawakupewa Notisi yoyote. Kuna takriban familia 200 ambazo zitakosa chakula, Karo za Shule na huduma za kimsingi ikiwa Wakenya hao maskini watafurushwa kwa nguvu kutoka eneo hili. Mali zao ziliharibiwa na kuteketezwa. Sasa hawana mbele wala nyuma,” Eric alisema.

Alienda mbele na kumtaka gavana Sakaja kuhakikisha kwamba wafanyibiashara hao wanapata sehemu mbadala ya kuendesha biashara zao ili kukimu familia zao wakati huu ambapo imekuwa vigumu kwa familia nyingi mijini na vijijini kuweka mlo mezani.

“Bwana Gavana @jsakaja nimeambiwa ni Maafisa wako waliokuja kuwahamisha. Wapatie sehemu mpya ya kufanyia biashara, Wajengee vibanda vya kufanyia biashara AU Waache peke yao,” Omondi aliwambia Sakaja.

Baadhi ya wafanyibiashara walisema kwamba wamekuwa wakifanya biashara ya kujipatia riziki kutoka sehemu hiyo kwa Zaidi ya miaka 15 na sasa wameona mtaji wao na familia zao zikilazimika kurudi katika uhayawinde kutokana na kitendo cha vibanda vyao kuangushwa.

 

View Comments