In Summary

• Mvulana wa Akothee, Evander Holifield Onyango alikuwa anahitimu na shahada ya uhandisi baada ya miaka 5 chuoni.

Akothee na Nelly Oaks.
Image: Insta

Mjasiriamali na msanii Akothee anazidi kuonyesha kwamba bado urafiki mkubwa unaweza ukaendelea baina ya watu wawili waliokuwa wapenzi baada ya penzi kuvunjika.

Hii ni baada ya msanii huyo mama wa watoto 5 kuandamana na aliyekuwa meneja na mpenzi wake Nelly Oaks katika sherehe ya mahafali ya mwanawe Akothee.

Mvulana wa Akothee, Evander Holifield Onyango alikuwa anahitimu na shahada ya uhandisi baada ya miaka 5 chuoni.

Katika sherehe hiyo, Akothee ambaye hujisifia na kujivunia kizazi chake aliandamana na bintiye Vesha Okello pamoja na Nelly Oaks licha ya kwamba wawili hao waliachana miaka michache iliyopita kabla ya Akothee kusonga mbele na maisha na hata kufunga harusi na Mzungu mwezi Aprili mwaka huu.

Akothee alijua kwamba watu watazua gumzo kuhusu kuonekana na Oaks na kutoa tahadhari kwa yeyeote ambaye atajaribu kumpangia maisha yake kuhusu ni nani wa kuonekana naye kwamba atamlisha block bila kusita.

“Nikiwasili kwenye sherehe ya mahafali ya mwanangu @holyfield_evander. Nikiwa na Familia yangu yote @veshashaillan na Rafiki Yangu Bora meneja wangu Osiepna @nellyoaks. Pigeni kelele mkinyamaza Niendelee kupost . Usitaje mwanaume mwingine kwa post ya mwingine ,hiyo ni kunipangia maisha na sipendi kupangiwa,” Akothee aliandika kwenye chapisho hilo.

Hii si mara ya kwanza kwa Nelly Oaks kuonesha ukaribu wake na familia ya Akothee licha ya kwamba uhusiano wao uligonga mwamba miaka kama miwili hivi iliyopita.

Wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja katika hafla za kualikwa kwac sherehe na tafrija maalum na hivyo kuwafanya wengi kuhisi kwamba huenda bado wanaendeleza uhusiano wao chini ya maji.

View Comments