In Summary

• Pia alikanusha kauli ya Diamond kwamba wimbo wa Shu ndio mkubwa Zaidi mitandoani kote, huku akimuonesha takwimu kwenye tiktok kwamba watu Zaidi ya milioni 1.8.

Diamond na Harmonize.
Image: Insta

Hata baada ya Baba Levo kumuombea msamaha kwa aliyekyuwa bosi wake Diamnond, msanii Harmonize haonekana kurudisha zana za vita stoo kwani ndio mwanzo ametangaza vita vya kibabe na Diamond.

Msanii huyo amemshambulia vikali Diamond kwa kujaribu kushindanisha wimbo wake wa Shu na ule wa Harmonize wa Single Again, ambao amekuwa akisisitiza kwamba ndio wimbo mkubwa Zaidi kuwahi kutoka ndani ya +255 katika mwaka huu wa 2023.

Harmonize alisema kwamba yeye haropokwi tu kama Diamond kwamba wimbo wake umepitwa kwa takwimu na ule wa Shu wake Diamond, bali anakwenda na takwimu zilizopo na ambazo mtu yeyote anaweza kuzihakiki.

“Karibia mwezi sasa na wimbo wa Single Again bado uko miongoni mwa ngoma 20 zilizosikilizwa Zaidi Afrika kwenye Spotify. Hakikisheni uongo haukudhalilishi. Ni ufinyu wa mawazo kushindanisha wimbo ulioimbwa Kizungu na ukawa hit duniani kote [Single Again] na kijimbo chako cha hovyo hovyo [Shu],” Harmonize alimwambia Diamond.

Pia alikanusha kauli ya Diamond kwamba wimbo wa Shu ndio mkubwa Zaidi mitandoani kote, huku akimuonesha takwimu kwenye tiktok kwamba watu Zaidi ya milioni 1.8.

Harmonize alisema kwamba ikiwa anadanganya basi yeyote atakayepata wimbo wa mwaka huu ambao umefanywa challenge tiktok zinazofika hata laki tano basi yeye yuko radhi kumpa zawadi ya shilingi milioni 10.

“Kazi kwenu wajuuzi kakusanyeni na jumulisheni nyimbo zilizotoka mwaka huu ukipata yenye laki 5 challenges tiktok basi njoo nikupe shilingi milioni 10,” alisema.

Alikwenda mbele kukiri kwamba hafanyi hivyo kwa sababu ya ulevi. Akisema “sijalewa mimi” na kudai kwamba hata kwenye jukwaa la YouTube ambalo wengi wanadhani ndiko kuna mafanikio ya kimuziki bado hakuna msanii anayemkaribia kwa takwimu.

Harmonize aligonga kwenye mshono akiita ngoma ya Shu ya Diamond kama ngoma uchwara ambayo haiwezi ikaifikia Single Again hata ikatuama vipi.

“Angalia sasa hata hapa YouTube ngoma ina Zaidi ya mara tatu ya kigoma chenu uchwara. Huwa mnakunywa nini kabla hamjaanza kuropokwa?” Harmonize alimuuliza Diamond na washikaji wake ambao wanajaribu kulinganisha Single Again na Shu.

View Comments